Na Humphrey Shao. Michuzi Tv Dar es Salaam
Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam Dr Toba Nguvila amewataka watumishi wote wa mkoa wa Dar es Salaam kuwa na mabadiliko ya kiutendaji na kuacha kufanya kazi kwa mazoea hili kuongeza ufanisi wa shughuli za Maendeleo katika mkoa huo .
Dr Toba amelazimika kusema hayo mara baada ya kuona kuna mwenendo wa kulegalega kwa shughuli za Maendeleo hasa ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Mchanganyiko ya mkoa inayojengwa Kigamboni ambapo amewataka wakurugenzi wote kuhakikisha wanaingiza fedha walizokubalina katika ujenzi wa shule hiyo kabla ya tarehe 30 may mwaka huu.
Dr Toba amesema hayo katika kikao chake Maalum cha Robo Robo ya Tatu ya mwaka ambacho kinajadili mwenendo wa bajeti na maadhimio na maelekezo yaliyo tolewa katika kukamilisha shughuli za Maendelo na miradi mbali mbali iliyopo katika Halmashauri zote za mkoa wa Dar es Salaam.
“Ni vyema kwa sasa kila mtu afikirie kubadilisha mwenendo wake wa ufanyaji kazi kwa kufuata mfumo unavyotaka, Sisi watendaji ndio tumepewa Dhamana ya kusimamia miradi hii ya Maendeleo hivyo tuna wajibu wa kuhakikisha miradi hii inamalizika kwa wakati hili kuweza kuleta heshima kwa serikali inayoongozwa na Rais Wetu Dk Samia Suluhu Hassan”
amesema kuwa moja ya Mradi wa Heshima katika mkoa wa Dar es Salaam amabo utaweza kuwatengenezea heshima watumishi wa mkoa huu ni kukamilika kwa shule ya Sekondari ya Mchanganyiko ya mkoa iliyopo kigamboni hivyo awezi kucheka na yoyote ambaye anapanga kuhujumu mradi huo.
ametaja kuwa ni vyema tukawa na kitu cha kumuonyesha Mh Rais katika Miaka hii minne ya Utawala wake Dar es Salaam tumefanya nini hivyo ni muhimu tukakamilisha shule hii mapema kwa kila anaepasa kutoa pesa atoe hili kufaniukisha ujenzi huu.