Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mha. Cyprian Luhemeja akifuatilia zoezi la usafishaji Ziwa Victoria katika eneo lililoathirika na Gugu Maji eneo la Busisi wilayani Sengerema hadi eneo la Kigongo Feri wilayani Misungwi mkoani Mwanza, Mei 15, 2025.
Zoezi hilo linaendelea kufanyika kwa njia mbalimbali kupitia vijana wanaokata kwa kutumia panga pamoja na Mtambo wa kusafisha na kuchimba kina cha maji ‘Watermaster’ ambao unauwezo wa kusafisha eka moja kwa siku.
Wakati zoezi hilo likiendelea tayari hatua zaidi zimeendelea kuchukuliwa ikiwa pamoja na ununuzi wa mitambo mitatu ambayo ipo katika hatua za awali.