Katika kuadhimisha Wiki ya Usalama Barabarani Duniani (May 12 – 18, 2025), kampuni ya Puma Energy Tanzania kwa kushirikiana na shirika la Amend Tanzania wameendesha ‘Mahakama Kifani ya Watoto’ kuhusu usalama barabarani tukio ambalo ni sehemu muhimu ya programu ya kampeni ya elimu ya usalama barabarani kwa shule za msingi ambayo pia inajulikana kama ‘Be Road Safe Africa’.
Awamu ya kwanza ya kampeni ya ‘Be Road Safe Africa’, ilitekelezwa mwaka 2023 and 2024, ambapo iliwafikia watoto zaidi ya 38,000 katika shule 20 za nchini Tanzania, Botswana, Zambia, na Zimbabwe.
Kampeni ya mwaka huu imewafikia zaidi ya wanafunzi 6,960 kupitia njia rahisi na shirikishi za kujifunzia, ikiwemo simulizi za hadithi, michezo – inayohusiana na masuala ya usalama barabarani na ‘Mahakama ya Watoto’.
Katika vifo 31 kwa kila watu 100,000, WHO inaripoti kwamba vifo vinavyotokana na ajali za barabarani nchini Tanzania ni karibu mara 1.7 ya kiwango cha kimataifa na juu zaidi ya wastani wa Afrika.
Programu ya ‘Be Road Safe Africa’ ni sehemu ya dhamira ya Puma Energy Tanzania ya kusaidia usalama na ustawi wa jamii, hasa jamii zilizo katika mazingira magumu na maeneo hatarishi.
Mwanafunzi wa darasa la saba katika Shule ya Msingi Kibugumo ya Kigamboni, Mohamed Abubakari Muhidin (13), wa kwanza kulia, akimhoji mmojawapo wa dereva aliyekamatwa nje ya barabara karibu na shule hiyo katika ‘Mahakama Kifani ya Watoto’ kwa kukiuka alama za barabarani ikiwa ni sehemu ya kampeni ya ‘Be Road Safe Africa’ inayoendeshwa na kampuni ya Puma Energy Tanzania na shirika la Amend nchini. Wakifuatilia kwa makini katikati ni Agness Daud Frank (13) na kushoto ni Munir Said Mussa (12). Awamu ya kwanza ya kampeni hiyo ya usalama barabarani mashuleni ilifanyika 2023 na 2024, kwa awamu ya pili mwaka huu imewafikia zaidi ya wanafunzi 6,960 katika shule tano za jijini Dar es Salaam ambazo ni Kisukuru (Tabata), Kunguru (Goba), Mjimpya (Kurasini), Ufukoni (Kigamboni), na Salasala (Salasala) kupitia njia rahisi na shirikishi za kujifunzia, ikiwemo simulizi za hadithi, michezo, mahakama kifani ya watoto na mashindano ya kuchora alama za usalama barabarani.
Wanafunzi wa darasa la saba katika Shule ya Msingi Kibugumo ya Kigamboni, kutoka kushoto, Abdulrazack Shaban Fundi (14), Nadya Salumu Abdallah (13), Munir Said Mussa (12), Agness Daud Frank (13), na Mohamed Abubakari Muhidin (13) wakimhoji mmojawapo wa dereva aliyekamatwa nje ya barabara karibu na shule hiyo katika ‘Mahakama Kifani ya Watoto’ kwa kukiuka alama za barabarani ikiwa ni sehemu ya kampeni ya ‘Be Road Safe Africa’ inayoendeshwa na kampuni ya Puma Energy Tanzania na shirika la Amend nchini. Awamu ya kwanza ya kampeni hiyo ya usalama barabarani mashuleni ilifanyika 2023 na 2024, kwa awamu ya pili mwaka huu imewafikia zaidi ya wanafunzi 6,960 katika shule tano za jijini Dar es Salaam ambazo ni Kisukuru (Tabata), Kunguru (Goba), Mjimpya (Kurasini), Ufukoni (Kigamboni), na Salasala (Salasala) kupitia njia rahisi na shirikishi za kujifunzia, ikiwemo simulizi za hadithi, michezo, mahakama kifani ya watoto na mashindano ya kuchora alama za usalama barabarani.
Mwanafunzi wa darasa la saba katika Shule ya Msingi Kibugumo ya Kigamboni, Mohamed Abubakari Muhidin (13), wa kwanza kulia, akimhoji mmojawapo wa dereva aliyekamatwa nje ya barabara karibu na shule hiyo katika ‘Mahakama Kifani ya Watoto’ kwa kukiuka alama za barabarani ikiwa ni sehemu ya kampeni ya ‘Be Road Safe Africa’ inayoendeshwa na kampuni ya Puma Energy Tanzania na shirika la Amend nchini. Wakifuatilia kwa makini kutoka kulia kwake ni Agness Daud Frank (13), Munir Said Mussa (12), Abdulrazack Shaban Fundi (14) na Nadya Salumu Abdallah (13). Awamu ya kwanza ya kampeni hiyo ya usalama barabarani mashuleni ilifanyika 2023 na 2024, kwa awamu ya pili mwaka huu imewafikia zaidi ya wanafunzi 6,960 katika shule tano za jijini Dar es Salaam ambazo ni Kisukuru (Tabata), Kunguru (Goba), Mjimpya (Kurasini), Ufukoni (Kigamboni), na Salasala (Salasala) kupitia njia rahisi na shirikishi za kujifunzia, ikiwemo simulizi za hadithi, michezo, mahakama kifani ya watoto na mashindano ya kuchora alama za usalama barabarani.
Mwanafunzi wa darasa la saba katika Shule ya Msingi Kibugumo ya Kigamboni, Munir Said Mussa (12), katikati, akimhoji mmojawapo wa dereva aliyekamatwa nje ya barabara karibu na shule hiyo katika ‘Mahakama Kifani ya Watoto’ kwa kukiuka alama za barabarani ikiwa ni sehemu ya kampeni ya ‘Be Road Safe Africa’ inayoendeshwa na kampuni ya Puma Energy Tanzania na shirika la Amend nchini. Wakifuatilia kwa makini kulia kwake kushoto kwake ni Agness Daud Frank (13) na Munir Said Mussa (12), na kulia kwake ni Nadya Salumu Abdallah (13) na Abdulrazack Shaban Fundi (14). Awamu ya kwanza ya kampeni hiyo ya usalama barabarani mashuleni ilifanyika 2023 na 2024, kwa awamu ya pili mwaka huu imewafikia zaidi ya wanafunzi 6,960 katika shule tano za jijini Dar es Salaam ambazo ni Kisukuru (Tabata), Kunguru (Goba), Mjimpya (Kurasini), Ufukoni (Kigamboni), na Salasala (Salasala) kupitia njia rahisi na shirikishi za kujifunzia, ikiwemo simulizi za hadithi, michezo, mahakama kifani ya watoto na mashindano ya kuchora alama za usalama barabarani.