Mkurugenzi Mkuu wa WCF Dkt.John Mduma akijibu maswali ya Wahariri na waandishi wa Habari kuhusiana mafanikio vya WCF katika kipindi cha Miaka minne ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Afisa Habari Mwandamizi wa Ofisi ya Msajili wa Hazina Sabato Kosuri akitoa maelezo kuhusiana na utaratibu wa mikutano kati ya wahariri na Taasisi za Umma zilizo chini ya Msajili wa Hazina.
Mkurugenzi Mkuu wa WCF Dkt.John Mduma akizungumza na Wahariri na waandishi wa Habari kuhusiana mafanikio vya WCF katika kipindi cha Miaka minne ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.

Baadhi ya wahariri katika mkutano wa WCF
*Yaahidi kuwafikia waajiri wote nchini.
Na Mwandishi Wetu
MFUKO wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) katika miaka Minne chini ya uongozi wa Rais Dkt.Samia Suluhu umeweza kutimiza malengo ya kuanzishwa kwa mfuko huo kwa kulipa fidia kwa wafanyakazi zaidi 19,659 na kufanya mfuko huo kuendelea kuwa imara kwa miaka 30 ijayo.
Hayo ameyasema Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo Dkt.John Mduma wakati akizungumza na wahariri wa vyombo vya Habari na waandishi katika mkutano ulioratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina ikiwa Taasisi na Mashirika yaliyo chini ya Ofisi ya Hazina kuzungumzia maendeleo ya Taasisi kwa ajili ya wananchi kupata taarifa na zinavyojiendesha,jijini Dar es Salaam.
Dkt.Mduma amesema kuwa mafanikio kwa taasisi hiyo katika miaka minne ni pamoja na kupata cheti cha ithibati cha ISO katika utoaji wa huduma kwa viwango vya Kimataifa.
Amesema kuwa katika utoaji wa huduma wamefanikiwa kutokana na kutumia mifumo ya Tehama kwa asilimia 90 ambapo walengwa hawana sababu ya kufika ofisi za WCF au kupeleka taarifa za maandishi katika karatasi.
Hata hivyo amesema kuwa agizo la Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ya kutaka mifumo ya Serikali isomane WCF imetekeleza hivyo kwa waajiri wote kuwasiliana kwa mifumo na changamoto kutatuliwa ndani ya mfumo na urasimu umepungua.
Dkt.Mduma amesema mafanikio hayo yanakwenda sambamba na maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwa mfuko huo.
Amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa mfuko huo wamefikia waajiri asilimia 94 ambapo wanakwenda katika mikakati ya kuwafikia wajasiriamali ambao wamesajiliwa katika mifumo rasmi ya utambuzi.
Aidha amesema kuwa tangu mfuko huo umeanzishwa umetoa fidia ya zaidi ya bilioni 100.
Amesema kuwa katika ufiadiaji wa matibabu kwa wafanyakazi WCF hawana kitita kwani nia kutaka kurejesha afya ya mfanyakazi aweze kuendelea kuzalisha na kujizalishia kipato.