Na.Ashura Mohamed -Arusha
Benki ya CRDB nchini imesema kuwa imefanikiwa kupandisha mapato yasiyotokana na Mikopo ambayo kwa mwaka 2024 yalikuwa chini tofauti na mwaka 2025 ambapo yamepanda na kufikia asilimia 47 hali ambayo inaifanya benki hiyo kuendelea kuwa kubwa na Imara zaidi.
Katika hatua hizo za ukuaji wa Benki hiyo ni lazima kuwa imara zaidi,kuwekeza zaidi kimtaji,kulinda uhimilivu zaidi,kulinda mtaji,na kuongeza umakini kwenye mikopo.
Akizungumza wakati wa mkutano mkuu wa 30 wa Wanahisa wa Benki ya CRDB,uliomalizika Jijini Arusha, Mkurugenzi wa benki hiyo bw.AbdulMajid Nsekela alisema kuwa kuimarika kwa taasisi hiyo ya fedha ni umakini na maono ambayo wamejiwekea kwa lengo la kuendelea kutoa huduma bora hapa nchini.
“Mtaji wetu sio mdogo sana na sio mkubwa sana tunaendelea kujiwekea malengo makubwa sana na tutayafikia ya kuwa benki bora barani Afrika,na ukiangalia ukuaji wetu ni asilimia 40 hadi 30 hivyo sio kiwango kidogo,na huduma zetu nyingi wateja wetu hawazipati mahali pengine hivyo tutaendelea kuboresha mtazamo wetu katika teknolojia ya kisasa na kuendelea kuimarika”Alisisitiza AbdulMajid
Katika hatua nyingine bw.AbdulMajid alitumia mkutano huo kuwatoa hofu wanahisa wa benki hiyo kuhusu uwekezaji uliofanyika katika nchi ya burudi ambapo alisema serikali ya nchi hiyo imefanya maboresho makubwa kwa kuruhusu biashara ya mabenki ndani ya nchi hiyo,hivyo kuwataka kuondoa wasiwasi.
Nae Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki hiyo Dkt.Ally Laay aliwashukuru wanahisa wa waliokubaliana na kwa kauli moja kuidhinisha Gawio la shilingi 65 kwa kila hisa, kiwango cha juu zaidi kuwahi kutolewa katika historia ya benki hiyo.
Aidha alisema Jumla ya Gawio lililotangazwa kwa mwaka fedha 2024 ni shilingi bilioni 170, ikionyesha uimara wa utendaji wa kifedha wa benki na dhamira yake ya kudumu ya kutoa thamani endelevu kwa wanahisa wake.
Nae Balozi wa Tanzania nchini Burundi mheshimiwa Gelasius Byakanwa akizungumza katika mkutano huo alisifu mageuzi makubwa ya benki hiyo kwa kuwa imekuwa ya mfano bora wa thamani kwa wanahisa na uadilifu wa kifedha.
Alisema benki hiyo imekuwa mfano bora wa thamani kwa wanahisa na uadilifu wa kifedha na rekodi yake ya kutoa gawio kila mwaka na utendaji wake mzuri katika soko la hisa ni ushahidi wa uongozi imara usio na kifani kwa kipindi Cha miaka 30.
Mwenyekiti Mstaafu wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Dkt. Ally Laay akizungumza katika mkutano mkuu wa 30 wa wanahisa wa benki hiyo uliofanyika katika ukumbi wa Simba uliopo katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC) .
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akizungumza katika mkutano mkuu wa 30 wa wanahisa wa benki hiyo uliofanyika katika ukumbi wa Simba uliopo katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC).