-Dkt. Samia Amefanya mambo makubwa ya maendeleo nchi nzima
Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), CPA Amos Makalla amesema Wilaya ya Muleba yenye majimbo mawili imefaidika na miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa hospitali ya wilaya, mradi mkubwa wa kutoa maji ziwa Victoria, uboreshaji wa bandarini ya Kemondo na umeme vijijini
Makalla ameeleza hayo leo Mei 19, alipokuwa akihutubia mkutano mkubwa wa hadhara katika viwanja vya Fatuma Wilaya ya Mubela mkoani Kagera akiwa katika muendelezo wa ziara yake ya siku saba katika mikoa ya kanda ya ziwa.
Aidha, CPA Makalla amemshukuru na kumpongeza Rais Dr Samia Suluhu Hassan,kwa kupeleka fedha nyingi za maendeleo nchini, akisistiza mahali popote palipo na changamoto zitatuliwa na serikali ya CCM kwa sababu wao ndiyo wenye dhamana na utatuzi wa changamoto za wananchi
“Miradi ya maji inaenda kutekelezwa mingi katika Wilaya ya Muleba walipita wakasema ziwa Viktoria lipo karibu wananchi wanashida ya maji ni waongo Sh bilioni 39 za mradi wa maji wa kimkakati unaenda kuchukuliwa ziwa Viktoria kuanza kutekekezwa katika Wilaya ya Muleba,” amesema Makalla.