NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV
OFISI ya Wakili Mkuu wa Serikali inatarajia kuendesha mafunzo kwa Mawakili wa Serikali kutoka Tanzania Bara na Visiwani Zanzibar ambapo mafunzo hayo yatafanyika Juni 2 hadi Juni 4, 2025 katika ukumbi wa mikutano wa AICC mkoani Arusha.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 28, 2025 Jijini Dar es Salaam, Wakili Mkuu wa Serikali Dkt. Ally Possi amesema mafunzo hayo yatawasadia Mawakili na wanasheria kufahamu mambo mbalimbali ikiwemo masuala ya uwekezaji na matumizi ya teknolojia katika kutekeleza majukumu yao.
“Ofisi kupitia mafunzo haya, itatoa elimu kwenye maeneo mbalimbali yatakayosaidia kuweka mazingira wezeshi ya biashara na uwekezaji, kwa kutoa mafunzo yatakayohusu mabadiliko ya sheria yatakayoendana na wakati tulionao”. Amesema Dkt. Possi.
Aidha amesema kuwa mafunzo hayo yatakagusa mbinu za kisasa zinazoendana na Dira ya maendeleo ya Taifa 2050 ambapo Mawakili watapata fursa ya kujifunza kupitia wataalamu wabobevu kutoka ndani na nje ya nchi yanayohusu nyanja ya kisheria.
Amesema mafunzo hayo yataendana na kikao cha pamoja na wakuu wa idara/ vitengo vya sheria kutoka ofisi zote za serikali ili kujadiliana kwa pamoja kuhusu uendeshaji wa mashauri ya madai na usuluhishi na kuimarisha mikakati ya kutoa huduma bora za kisheria kwa niaba ya Serikali na taasisi zake.
Pamoja na hayo amesema kuwa katika kilele cha mafunzo hayo, ofisi itazindua mfumo wa menejimenti ya taarifa za mashauri “Case Management Information System- CIMS” ambao unasajili mashauri yanayopokelewa ofisini, kuhifadhi taarifa mbalimbali za mashauri na takwimu za aina ya mashauri yanayoendeshwa kwa kipindi husika.
Mafunzo hayo yatafunguliwa na Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro ambapo Kauli Mbiu ya Mafunzo hayo ni “Ubobezi wa Kisheria kwa ajili ya Kesho: Teknolojia, Mikakati na Mizania Binafsi kwa Mawakili wa Serikali katika kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050”.
Wakili Mkuu wa Serikali Dkt. Ally Possi akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 28, 2025 Jijini Dar es Salaam, akitoa taarifa kuhusu ofisi hiyo kuandaa mafunzo kwa Mawakili wa Serikali kutoka Tanzania Bara na Visiwani Zanzibar ambapo mafunzo hayo yatafanyika Juni 2 hadi Juni 4, 2025 katika ukumbi wa mikutano wa AICC mkoani Arusha.

Baadhi ya Mawakili wa Serikali wakiwa katika Mkutano wa Wakili Mkuu wa Serikali na waandishi wa habari leo Mei 28, 2025 Jijini Dar es Salaam.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)