Itifaki ya Haki za Watu Wenye Ulemavu Afrika (The African Disability Protocol – ADP) ni mfumo wa kisheria unaoshughulikia ubaguzi wa kipekee unaowakabili watu wenye ulemavu barani Afrika. Mnamo 2018, Baraza Kuu la Umoja wa Afrika lilipitisha ADP. Tangu wakati huo, Angola, Burundi, Cameroon, Jamhuri ya Kongo, Kenya, Mali, Malawi, Msumbiji, Namibia, Nigeria, Niger, Rwanda, Afrika Kusini, Sahrawi Arab Democratic Republic and Uganda zimeridhia. Ili ADP ianze kutumika, angalau nchi wanachama 15 lazima zitie saini na kuiridhia; hadi sasa, tayari imeanza kutumika. Kampeni ya #Ridhia ADP inatoa wito kwa serikali zote barani Afrika kuendeleza na kulinda haki za watu wenye ulemavu.
Kuidhinishwa kwa Itifaki ya Haki za Watu wenye Ulemavu Afrika (ADP) kutanufaisha sana Watanzania, hasa watu wenye ulemavu. Faida moja kuu ni kuanzisha mfumo imara wa kisheria ambao unakuza sheria na sera jumuishi zinazofaa kwa muktadha wa kitaifa. Uidhinishaji huu utaongeza ari ya Tanzania katika kulinda haki za watu wenye ulemavu. Zaidi ya hayo, itawawezesha watu wenye ulemavu katika sekta mbalimbali, ikiwa ni pamoja na elimu, huduma za afya, ajira, na miundombinu, kuhakikisha fursa sawa na kukuza ushirikishwaji katika nyanja za kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni.
Video ya uhamasishaji kuhusu ADP inalenga kuonyesha umuhimu wa Itifaki ya Ulemavu ya Afrika (ADP), ikitoa nafasi kwa sauti za watu wenye ulemavu kote Tanzania, ikiwemo Zanzibar na Bara. Inaunga mkono kuridhiwa kwa ADP, ikisisitiza umuhimu wake kwa jamii ya Tanzania. Video hii inazungumza moja kwa moja na wafanya maamuzi, watu wenye ulemavu, na jamii kwa ujumla, ikisisitiza kwamba uridhiwaji wa ADP si kwa ajili ya watu wenye ulemavu pekee, bali ni juhudi za pamoja zitakazobadilisha sera na mwelekeo wa kitaifa kuelekea jamii jumuishi.