

*Dkt.Kirama aweka mikakati kutoa Mawasiliano ya Internet kwa gharama nafuu
Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
UONGOZI wa Makao Makuu ya Internet Society kutoka Marekani umetembelea Tanzania kuangalia shughuli zinazotekelezwa na Chapter ya Tanzania ikiwemo mradi wa Intaneti kwa jamii unafanyika katika Wilaya ya Kigamboni
Akizungumza na Waandishi wa Habari Rais wa Internet Society Tanzania Chapter Dkt.Nazar Kirama amesema ujio huo ni fursa kwa nchi katika kuendelea kutanua uwigo wa matumizi ya Internet pamoja na Elimu ya Kidigitali.
Kirama amesema pamoja na ugeni huo wametembelea Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT) kutokana na kuwa mfumo wa utoaji wa elimu kwa masafa ya Internet hivyo Internet Society ndio sehemu wanaangalia katika kutumia vituo hivyo katika kuweka internet kwa ajili ya kupeleka internet kwa jamii.
Katika ziara hiyo wametembelea mradi wa Internet wa Shule ya msingi Ufukoni na Sekondari Paul Makonda ambao umeunganisha na huduma zingine za kijamii kwa gharama nafuu.
Amesema upatikanaji wa gharama nafuu unatokana idadi ya wanaojiunga kutumia huduma gharama zake zinashuka kwa kiasi kikubwa.
Hata hivyo amesema kuwa kutokana na Internet Society katika mikakati walioiweka ni kuhakikisha kila mtu anapata huduma ya internet bila kikwazo na kwa agharama nafuu.
Dkt.Kirama amesema kuwa makubaliano na OUT ni fursa kubwa kwa jamii zinazozunguka vituo vyake kupata huduma ya mawasiliano ya Internet.