Na Jane Edward, Arusha
Asasi za kiraia nchini Tanzania zinatarajia kuanza Wiki ya AZAKI 2025 (CSO Week 2025), itakayo jadili Dira ya maendeleo ya Taifa pamoja na kuwakutaniaha wadau Mbalimbali ambapo zaidi ya washiriki 800 wanatarajiwa kushiriki.
Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Wiki ya AZAKI na Mkurugenzi Mkazi wa CBM International Tanzania Nesia Mahenge amesema tukio hilo litafanyika kuanzia tarehe 2 hadi 6 Juni 2025 katika Hoteli ya Mount Meru, Arusha na kusisitiza umuhimu wa tukio hilo kama fursa ya kutathimini safari ya pamoja katika kushughulikia changamoto za ndani, na kuandaa mikakati ya pamoja kwa ajili ya maendeleo ya taifa.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya FCF na Rais wa Tanzania Women Chamber of Commerce (TWCC) CPA Mercy Sila, ametoa rai kwa vijana na Wanawake kushiriki na kutoa maoni yao kuhusu masuala ya maendeleo.
Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation for Civil Society (FCS).Justice Rutenge amesema kuwa CSO Week 2025 ni tukio la kitaifa linalotoa fursa kwa Watanzania kushiriki katika kutoa maoni yao kuhusu Dira ya maendeleo 2050.
Kwa upande wake Adamsoni Nsimba Katibu Mkuu wa Baraza la Asasi za Kiraia, ameeleza kuwa asasi za kiraia ni washirika muhimu katika kuunda sera za umma na kulinda haki za walaji, na kwamba Vision 2050 haiwezi kufanikiwa bila ushiriki wa wananchi kupitia asasi hizo.
Mwisho…