Na: Humphrey Shao, Michuzi Tv
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru ndugu Ismail Ussi Leo tarehe 3 June 2025, amezindua mradi wa Nishati Safi katika Soko la Samaki Ferry
Akizungumza na wananchi na wafanyabiashara wa soko la samaki Feri ndugu Ismail Ussi amesisitiza umuhimu wa kuachana na matumizi ya nishati chafu kama mkaa na kuni, huku akihimiza jamii kutumia nishati safi
“ Tumeona juhudi kubwa zinazofanywa na Mheshimiwa Rais Samia katika kuhakikisha Watanzania wanapata nishati safi ya kupikia. Kupitia mikakati na sera madhubuti, Serikali imerahisisha upatikanaji wa gesi majumbani na kuwekeza kwenye teknolojia rafiki kwa mazingira. Hii ni ishara ya uongozi wenye maono na kujali maisha ya wananchi.”
Mradi huu umetekelezwa kwa ushirikiano kati ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na Kampuni ya Oryx Gas kwa gharama ya Shilingi milioni 216.
Mradi unalenga kupunguza matumizi ya mkaa na kuni, kulinda afya, kupunguza gharama kwa wajasiriamali, na kuhifadhi mazingira.
“Jitokeze Kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kwa Amani na Utulivu “
KAULI MBIU: “Jitokeze kushiriki Uchaguzi Mkuu
wa Mwaka 2025 kwa Amani na Utulivu”