Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Hamza S. Johari
amewakumbusha Mawakili wa Serikali juu ya wajibu wao na masuala muhimu
yanayohusu majadiliano ya mikataba mbalimbali ambayo Serikali au Taasisi
inakusudia kuingia au ina maslahi nayo.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameyasema hayo tarehe 4 Juni,
2025 wakati akiwasilisha mada kuhusu mbinu za kufanya Majadiliano ya Mikataba
na namna ya Kuunganisha Utaalamu wa Kisheria na Ujuzi wa Biashara kwa washiriki wa mafunzo kwa Mawakili wa
Serikali yaliyoandaliwa na kuendeshwa na Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali
yanayofanyika Jijini Arusha.
Akitoa mada katika mafunzo hayo, Mwanasheria Mkuu wa
Serikali amesema kuwa ni muhimu kwa mawakili wa Serikali kuzingatia umakini,
weledi na uzalendo wakati wanashiriki majadiliano ya mikataba mbalimbali yenye
maslahi Serikali na taifa kwa ujumla.
“Kutokana na unyeti wa majukumu ya Mawakili wa Serikali
katika masuala ya mikataba hivyo ni muhimu kwa Mawakili kuzingatia weledi na
kutanguliza uzalendo wakati wanashiriki kwenye majadiliano ya mikataba
mbalimbali.” Amesema Mwanasheria Mkuu wa Serikali
Aidha, Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameongeza kuwa Ofisi ya
Mwanasheria Mkuu wa Serikali iko tayari kutoa ushauri na msaada wa kisheria kwa
Mawakili wa Serikali wakati wowote ili kuwarahisishia Mawakili wa Serikali
utekelezaji wa majukumu mbalimbali hususani wakati wa majadiliano ya Mikataba.
“Sisi Ofisi ya Mwanasheria Mkuu tunawaahidi ushirikiano wa
kutosha mara zote mnapohitaji ushauri wa kisheria, lengo letu ni kufanya
majadiliano ya mikataba mbalimbali yanakuwa na tija kwa taifa na Wananchi
wake.” Amesema Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Kwa upande wake, Wakili wa Serikali Bi. Asia Juma
amefurahishwa na mada zilizotolewa kwenye mafunzo hayo huku akieleza kuwa mada
iliyowasilishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali imewaongezea maarifa zaidi
watakayowatumia katika kuboresha utendaji kazi wao.
*“Tunamshukuru sana Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa
wasilisho lake wasilisho lililosheheni masuala muhimu kuhusiana na majadiliano
ya mikataba, naamini sisi mawakili tumejifunza mengi