MWENYEKITI wa GIDESHA AMCOS, Bw. Hipoliti Umbu,akitoa Pongezi kwa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) baada ya kupatiwa mafunzo kwa wanachama wa Vyama vya Ushirika vya Mazao ya Bustani ikiwa ni utekelezaji wa Mradi Kwa awamu ya pili mwaka 2024/2025 katika Kijiji Cha Simhha Halmshauri ya Wilaya ya Mbulu mkoani Manyara.
Na.Alex Sonna-HAYDOM
Mwenyekiti wa GIDESHA AMCOS, Hipoliti Umbu, amesema kuwa mafunzo ya ushirika waliyopatiwa na Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) yanaenda kuleta mabadiliko makubwa ya kifikra na yanaenda kuibua mapinduzi ya maendeleo kiuchumi kwa wanachama wa Vyama vya Ushirika vya Mazao ya Bustani na jamii kwa ujumla.
Umbu ameyasema hayo wakati wa mafunzo kwa wanachama wa Vyama vya Ushirika vya Mazao ya Bustani ikiwa ni utekelezaji wa Mradi wa awamu ya pili mwaka 2024/2025 yaliyofanyika leo Juni 5, 2025 katika Kijiji cha Simhha Halmshauri ya Wilaya ya Mbulu mkoani Manyara.
“Katika hali ya sasa, elimu hii ikiwa itachukuliwa kwa uzito, ifikapo mwaka 2026 tutashuhudia mabadiliko makubwa kwa wanachama wetu na jamii nzima inayotuzunguka,” amesema Umbu.
Amesema kuwa chama cha GIDESHA AMCOS kilianzishwa rasmi mwezi Desemba miaka miwili iliyopita na mwaka jana walianza rasmi kujiunga na mfumo wa stakabadhi ghalani, mfumo ambao licha ya kuleta mapato kidogo kwa awamu ya kwanza, uliweza kuhamasisha wanachama wengine kujiunga kutokana na mafanikio yaliyoonekana.
“Mwaka huu tayari tumeanza tena shughuli kwa kasi zaidi na tumeletewa mizani ya kidigitali, jambo ambalo litatusaidia sana kuzuia unyonyaji kwa wakulima, hasa kwenye suala la upimaji wa mazao,” ameongeza Umbu.
Aidha, Umbu ametumia nafasi hiyo kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuonesha dhamira ya kweli ya kuwaendeleza wakulima, hasa kwa hatua yake ya hivi karibuni ya kuzindua Benki ya Ushirika ambayo imewawezesha wanachama kufungua akaunti na kuanza mchakato wa kununua hisa katika benki hiyo.
Kwa upande wake, Afisa Kilimo kutoka Wizara ya Kilimo, Bahati Majaliwa, amesema kuwa kupitia Tume ya Maendeleo ya Ushirika, serikali inaendelea na juhudi za kutoa elimu kwa wanachama wa vyama vya ushirika ili kuongeza uelewa wa majukumu yao na manufaa ya kushiriki kikamilifu katika mfumo wa ushirika.
“Lengo la mafunzo haya ni kuhakikisha kuwa kila mwanachama anajua nafasi yake na wajibu wake ndani ya chama, pamoja na kuelewa dhana pana ya ushirika kama njia ya kujikwamua kiuchumi,” amesema Majaliwa.
Naye Mkufunzi wa Kilimo na Mwezeshaji Masoko kutoka Chuo cha Uhaulishaji Teknolojia Mazao ya Bustani (HORTI- TENGERU), Abdallah Mussa, amesema kuwa mafunzo hayo ya siku mbili yana lengo la kuwajengea uwezo wanachama wa vyama vya ushirika ili waweze kulima kwa tija na kupata faida kubwa.
“Tumejikita zaidi katika kuwasaidia wanachama kuelewa umuhimu wa kufanya utafiti wa soko kabla ya kuzalisha. Dhana hii ni nyenzo muhimu ya kuingia kwenye mnyororo wa thamani wa mazao yao,” amesema Mussa.
MWENYEKITI wa GIDESHA AMCOS, Bw. Hipoliti Umbu,akitoa Pongezi kwa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) baada ya kupatiwa mafunzo kwa wanachama wa Vyama vya Ushirika vya Mazao ya Bustani ikiwa ni utekelezaji wa Mradi Kwa awamu ya pili mwaka 2024/2025 katika Kijiji Cha Simhha Halmshauri ya Wilaya ya Mbulu mkoani Manyara.
Mkufunzi wa Kilimo na Mwezeshaji Masoko kutoka Chuo cha Uhaulishaji Teknolojia Mazao ya Bustani (HORTI- TENGERU), Abdallah Mussa,akiwasilisha mada wakati wa mafunzo kwa wanachama wa Vyama vya Ushirika vya Mazao ya Bustani ikiwa ni utekelezaji wa Mradi Kwa awamu ya pili mwaka 2024/2025 katika Kijiji Cha Simhha Halmshauri ya Wilaya ya Mbulu mkoani Manyara.
Afisa Kilimo kutoka Wizara ya Kilimo, Bahati Yusuph Majaliwa,akiwasilisha mada wakati wa mafunzo kwa wanachama wa Vyama vya Ushirika vya Mazao ya Bustani ikiwa ni utekelezaji wa Mradi Kwa awamu ya pili mwaka 2024/2025 katika Kijiji Cha Simhha Halmshauri ya Wilaya ya Mbulu mkoani Manyara.
SEHEMU ya washiriki wa Gidesha AMCOS wakifatilia mada mbalimbali wakati wa mafunzo kwa wanachama wa Vyama vya Ushirika vya Mazao ya Bustani ikiwa ni utekelezaji wa Mradi Kwa awamu ya pili mwaka 2024/2025 yaliyofanyika leo Juni 5,2025 katika Kijiji Cha Simhha Halmshauri ya Wilaya ya Mbulu mkoani Manyara.

Diwani wa Kata ya Haydarer, Anna Sulle,akiipongeza Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) kwa kuwapatia mafunzo wanaushirika wa Gidesha AMCOS mara baada ya mafunzo kwa wanachama wa Vyama vya Ushirika vya Mazao ya Bustani ikiwa ni utekelezaji wa Mradi Kwa awamu ya pili mwaka 2024/2025
AFISA Ushirika Mwandamizi kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) Bi.Happyness Olotu,akihitimisha mafunzo kwa wanachama wa Vyama vya Ushirika vya Mazao ya Bustani ikiwa ni utekelezaji wa Mradi Kwa awamu ya pili mwaka 2024/2025 katika Kijiji Cha Simhha Halmshauri ya Wilaya ya Mbulu mkoani Manyara kwa wanaushirika wa Gidesha AMCOS