MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mary Chatanda, amewasihi wananchi hususan wanawake kujitokeza kwa wingi katika uchsguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu.
Amesema ni haki ya Kila mtanzania kushiriki katika uchaguzi huo na kuwachagua Viongozi watakaochagiza juhudi za maendeleo zinazofanywa na serikari chini ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan, kuwaletea maendeleo.
Chatanda ameyasema hayo wlayani Mkuranga, mkoani Pwani katika ziara yake ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM.
Katika ziara hiyo ameambatana na Makamu Mwenyekiti wa UWT Zainab Khamis Shomari na Wajumbe wa Kamati Tendaji wa umoja huo na Wajumbe wa Baraza Kuu la UWT.
Amesema Rais Dk Samia , ametoa fedha nyingi za maendeleo mkoani humo, hivyo ziara hiyo ililenga kujiridhisha na maendeleo yaliyofanywa.
Pia kuielezea Ilani mpya ya CCM kwa 2025/2030 kwa wananchi hivyo kuwasihi kujitokeza kupiga kura Oktoba ili kuwachagua Viongozi sahihi katika maeneo yao.
Akitoa salamu kwa Mwenyekiti wa UWT, Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Khadija Nasri, amesema kwa asilimia kubwa miradi iliyoanishwa kwenye Ilani ya CCM imetekelezwa kikamilifu hivyo wana kila sababu ya kumshukuru. Rais Dk. Sami.
Jumla ya miradi 39 yenye thamani ya zaidi ya sh. bilioni 500 imetekelezwa na kukaguliwa na viongozi hao WA UWT wilayani humo.