Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akifanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mhe. Antonio Guterres kabla ya mazungumzo yao yaliyofanyika kando ya Mkutano wa Tatu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Bahari unaofanyika Jijini Nice nchini Ufaransa leo tarehe 10 Juni 2025. Mazungumzo hayo yamelenga kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na Umoja wa Mataifa kupitia Taasisi mbalimbali zilizo chini ya umoja huo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisalimiana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mhe. Antonio Guterres kabla ya mazungumzo yao yaliyofanyika kando ya Mkutano wa Tatu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Bahari unaofanyika Jijini Nice nchini Ufaransa leo tarehe 10 Juni 2025.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akimkabidhi Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mhe. Antonio Guterres zawadi ya mfano wa mlango maarufu unaopatikana Zanzibar pamoja na viungo mbalimbali vya vyakula mara baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika kando ya Mkutano wa Tatu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Bahari unaofanyika Jijini Nice nchini Ufaransa leo tarehe 10 Juni 2025.