VICTOR MASANGU, KIBAHA
Jumuiya ya umoja wa wanawake (UWT) Wilaya ya Kibaha mjini katika kuunnga juhudi za Rais awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kutekeleza ilani ya chama kwa vitendo imefanikiwa kuanzisha mradi wa mgahawa ikiwa kama ni moja ya kitega uchumi kwa ajili ya kuweza kujikwamua kiuchumi pamoja na mradi wa ujenzi wa nyumba ya Katibu wa jumuiya hiyo.
Hayo yamebainishwa na Katibu wa UWT Wilaya ya Kibaha mjini Cecilia Ndaru wakati wa kikao cha kikanuni cha baraza hilo ambacho kimeweza kukutana kwa lengo la kujadili masuala mbali mbali ya kimaendeleo, kujiandaa katika kuelekea uchaguzi mkuu, mapokezi ya Mwenyekiti wa UTW Taifa sambamba na kupokea taarifa ya utekelezaji wa ilani ya chama kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2020 hadi 2025 kutoka kwa madiwani wa viti maalumu.
Katibu Ndaru amesema kwamba lengo lao kubwa ni kuweka mikakati madhubuti ya kuendelea kubuni na kunzisha miradi mipya ambayo itaweza kuwa ni mkombozi mkubwa kwa jumuiya hiyo kuweza kujiongezea kipato pamoja na kuweka misingi imara ya kuweza kuimarisha jumuiya hiyo kuanzia ngazi za chini.
Katika kikao hicho cha baraza ambacho kilifunguliwa na Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) Mwalimu Mwajuma Nyamka ambaye alikuwa mgeni rasmi amewataka wanawake hao kuhakikisha wanakuwa naa umoja na mshikamano hasa katika kioindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.
Nyamka katika baraza hilo amewahimiza wanawake kuchangamkia fursa za kugombea nafasi mbali mbali za uongozi ikiwemo katika nafasi ya udiwani pamoja na ubunge na kuwaomba wanampa kura nyingi za kishindo cha hali ya juu Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan katika uchaguzi huo mkuu amebainisha kwamba lengo la chama ni kuhakikisha wanashinda katika nafasi zote.
“Nawapongeza sana wanawake wa UWT Wilaya ya Kibaha mjini kwa kuweza kuchapa kazi kwa bidii na mimi nimefaarijika sana kuona meweza kusimamia vemaa utekelezaji wa ilani ya chama na pia mmeweza kuanzisha mradi wa mgahawa amabo utaweza kuwa ni chachu ya kujikwamua kuchumi sambamba na ujenzi wa nyumba ya katibu kwa hivyo kitu kikubwa mfanye kazi na viongozi ambao bado wapo madarakani achanane na kampeni amabzo hazina faida kwa kipindi hiki,”amebainisha Nyamka.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Kibaha mjini Elina Mgonja amempongeza kwa dhati Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu kwa kuweza kutenga fedha nyingi ambazo zimekwenda katika kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo sekta ya elimu, afya, maji,miundombinu ya barabara pamoja na huduma nyingine za kijamii.
Aidha Mgonja amemshukuru Mbungu wa Jimbo la Kibaha mjini Mhe. Silvestry Koka pamoja na mke wake Mama Selina Koka kwa kuweza kuwa mstari wa mbele kupambana katika kuwasaidia kwa hali na mali kufanikiwa ujenzi wa mradi wa mgahawa pamoja na mradi wa ujenzi wa nyumba ya katibu wa UWT kwa kushirikiana na wadau na viongozi wengine wa chama pamoja na jumuiya zake.
Naye mlezi wa UWT Wilaya ya Kibaha mjini ambaye pia ni mke wa Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Mama Selina Koka amewahimiza wanawake wote kuwa na umoja na mshikamano hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 na kuwaomba kuwa mstari wa mbele katika kupiga kura lengo ikiwa ni kuweza kushika katika nafasi zote za udiwani, ubunge, pamoja na nafasi ya urais.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka ambaye amefunga rasmi kikao cha baraza hilo ameishukuru kwa dhati jumiya hiyo ya wanawake kwa kuweza kumpa ushirikiano na sapoti kubwa katika kipindi chote ambacho aliingia madarakani na kuahidi kuendelea kushirikiano nao katika masuala mbali mbali ya kimaendeleo na kutatua changamoto ambazo wanakumbana nazo.
Koka amebainisha kwamba tangu aingie madarakani mnamo mwaka 2010 ameweza kuwa bega kwa bega na jumuiya ya UWT ambapo wameweza kushirikiana katika baadhi ya miradi mbali mbali ikiwemo ujenzi wa mradi wa nyumba ya Katibu pamoja naa kiteega uchumi cha mgahawa sambamba na kushirikishwa katika vikao mbali mbali vyebye kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo ikiwemo kutatua kero na changamoto za wananchi.