Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma
Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum Dkt. John Jingu ametoa wito kwa jamii kupokea kwa mtazamo chanya jitihada na mipango ya Serikali katika kutekeleza program ya Kizazi chenye Usawa kwa kila mmoja kutimiza wajibu wake katila mahali alipo.
Hayo yameyaeleza hayo leo hii Jijini Dodoma Juni 12,2025 na Merikion Ndofi aliyemuwakilisha Katibu Mkuu huyo wakati akifungua mafunzo ya kujengewa uelewa kwa Maafisa Habari wa Mikoa 26 ya Tanzania kuhusu utekelezaji wa Programu ya Kizazi chenye Usawa.
Na kuongeza kuwa jamii ipokee kuwa mipango hiyo ni yakuleta usawa kati ya wanawake na wanaume na sio yenye kuwaacha wanaume kwani wanaume tayari wako juu hivyo Serikali inawainua wanawake ili kuleta usawa.
“Wito wangu kwa jamii iwe na mapokeo chanya katika mipango ya Serikali na isaidie kuhakikisha kwamba kila mmoja anatimiza wajibu wake sehemu alipo”.
“Jamii ipokee kwamba hiyo ni mipango tu ya kuleta usawa kati ya wanawake na wanaume na siobkwamba Serikali inawaacha wanaume, kwani wanaume mpaka sasa wapo juu kidogo ukilinganisha na wanawake ambapo Serikali sas unawainua waliokuwa chini ili kuleta usawa “.
Aidha akielezea mafaniko ya Programu hiyo tangu kuanzishwa kwake mnamo Julai 2021,amesema kumekuwa na mafanikio makubwa yanayoonesha jinsi Serikali inavyoendeleza mipango hiyo inayopelekea wanawake kushikiria Uchuni,idadi kuongezeka katika masomo kuanzia ngazi ya msingi hadi vyuo vikuu lakini pia katika biashara zilizo rasmi na zisizo rasmi bado wanawake wamejitokeza na kufanya vizuri.
Naye Juliana Kibonde ambaye ni Mkurugenzi msaidizi idara ya Maendeleo ya jinsia sehemu ya Wanawake amesema kuwa wamewaita Maafisa Habari hawa kutoka Mikoa yote Tanzania ili kuwajengea uelewa wa kuunganisha Habari na jitihada za Serikali zinazofanyika katika kumkwamua mwanamke na kuwezesha wanawake kiuchumi.
Na kuona jinsi gani wataweza kuunganisha hizo Habari ambazo zote zinalenga kumuwesha mwanamke kama vile asilimia 10 na majukwaa ya uwezeshaji wanawake kiuchumi na kuoanisha na habari za jukwaa la kizazi chenye usawa.
Na kueleza kuwa baada ya mafunzo haya anaamini kuwa habari zitakazokuwa zinatoka za uwezeshaji wanawake kiuchumi zitakuwa zimeunganushwa kabisa na jukwaa la kizazi chenye uswa na zenye kuonesha jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuleta usawa wa kijinsia hapa Nchini.
Akitoa salamu za Mkoa mwenyeji Afisa Habari wa Mkoa wa Dodoma Bi Francisca Mselemu amesema kwa niaba ya wengine wanaahidi kutumia nguvu waliyonayo ili jambo hili kupata muitikio uliokusudiwa na kupata kitu kikubwa kitakachowawezesha kuendelea kwani wao ni jeshi kubwa.
Mafunzo haya yalilenga Maafisa Habari wa Mikoa yote 26 ya Tanzania lakini wamehudhuria Maafisa wa Mikoa 22 ikisalia mikoa 4 ambayo wawakilishi wake hawakuweza kufika kutokana na dharula mbalimbali.