Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Taifa Ndg. Mohammed Ali Kawaida apokelewa Kwa kishindo na Vijana wa CCM Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi leo Ijumaa 13 Juni, 2025.
Mwenyekiti anaendelea na Ziara yake ya Siku tatu za Kibabe inayohitimishwa leo katika Mkoa wa Katavi baada ya kutembelea wilaya za Mlele, Tanganyika na leo Mpanda.
Ziara yake imelenga kukagua uhai wa chama na Jumuiya, Utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi 2020-2025 sambamba na maandalizi ya uchaguzi mkuu 2025.