VIVO Energy Tanzania, kampuni inayosambaza na kuuza mafuta na vilainishi vya chapa ya Shell, inajivunia kutangaza uzinduzi wa kampeni yake iitwayo “Uliza Oili ya Shell.” Hii ni harakati thabiti na ya kina inayolenga kuwaelimisha na kuwawezesha madereva wa Tanzania kufanya maamuzi sahihi kuhusu vilainishi wanavyotumia—ikichochea ulinzi wa injini na pia maendeleo ya kijamii.
Kampeni hii ilizinduliwa katika hafla iliyofanyika katika makao makuu ya kampuni hiyo yaliyopo Masaki, Dar es Salaam. Inawalenga madereva, waendesha bodaboda, mafundi na wasafirishaji, ikisisitiza umuhimu wa kutumia vilainishi halisi vya Shell ili kuboresha utendaji wa injini, kupunguza gharama za matengenezo, na kuongeza ufanisi wa injini pamoja na matumizi ya mafuta.
Akizungumza wakati wa uzinduzi, Bw. Mohamed Bougriba, Mkurugenzi Mtendaji wa Vivo Energy Tanzania, aliwakaribisha wageni na kusisitiza dhamira ya kina ya kampeni hiyo:
“Tunafurahi sana leo kuwakaribisha katika tukio la uzinduzi wa ‘Uliza Oili ya Shell,’ kampeni jumuishi inayolenga kuwasaidia madereva na mafundi nchini Tanzania kwa suluhisho za vilainishi vya injini vinavyoaminika na vyenye ubora wa juu, ambavyo vinaboresha utendaji na kudumu kwa muda mrefu.”
“Kupitia kampeni hii, tunathibitisha tena ahadi yetu ya kutoa teknolojia ya kiwango cha kimataifa kupitia vilainishi vya Shell ambayo inalinda injini, inapunguza gharama za matengenezo, na huongeza ufanisi wa mafuta – ikileta thamani halisi kwa watumiaji wetu.”
Bw. Bougriba pia alitoa shukrani kwa wateja wa vilainishi vya Shell duniani kote:
“Tunawashukuru wateja wote waliotuwezesha kuwa chapa namba moja ya vilainishi duniani kwa miaka 18 mfululizo – mafanikio yanayotokana pia na ushirikiano wetu imara na watengenezaji wakubwa wa magari duniani.”
Aidha, alitangaza hatua muhimu ya ushirikiano:
“Tunajivunia kuanzisha ushirikiano wa kimkakati na VETA ili kuwapatia vijana wa Kitanzania ujuzi muhimu wa huduma za vilainishi – hatua itakayofungua fursa za ajira na ujasiriamali. Tunawapongeza pia wahitimu wa VETA waliopo hapa leo, kama ushahidi wa matokeo chanya ya haraka kufuatia kusainiwa kwa Mkataba wa Makubaliano (MOU).”
“Katika Vivo Energy, tunawekeza katika watu, ushirikiano, na utendaji – nguzo kuu za maendeleo endelevu na maendeleo ya taifa.”
“Kama methali ya Kiswahili inavyosema, ‘Samaki mkunje angali mbichi,’ inasisitiza umuhimu wa kuwaendeleza vijana mapema kwa mafanikio ya kudumu. Na kama alivyosema Mwalimu Julius Nyerere, ‘Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu. Tunapofanya kazi pamoja, tunajenga jamii yenye maendeleo na mafanikio kwa wote.’ Kwa ushirikiano, tunajenga jamii yenye mafanikio.”
Kampeni ya “Uliza Oili ya Shell” inahusisha bidhaa tatu kuu za vilainishi vya Shell, kila moja ikiwa imeundwa mahsusi kwa mahitaji ya injini tofauti:
Shell Advance – Kwa pikipiki, bodaboda na bajaji; Ulinzi wa kipekee wa injini – wakati wowote,popote
Shell Helix – Kwa magari yenye injini za petroli; huleta nguvu zaidi,uchakavu pungufu- kwa kila safari ya thamani
Shell Rimula – Kwa magari ya dizeli kama malori, mabasi na dala dala; hutoa ulinzi wa injini bila mashaka, kwa safari za uhakika
Bw. Godwin Mwita, Mkuu wa idara ya biashara na vilainishi Vivo Energy Tanzania, aliongeza:
“Vilainishi vyetu vinatoa ulinzi wa muda mrefu na utendaji wa kipekee wa injini. Tunapambana kikamilifu dhidi ya bidhaa bandia ili kuwalinda watumiaji wetu, na tunapanua mtandao wetu wa usambazaji ili kuhakikisha vilainishi vya Shell vinapatikana kote nchini – mijini na vijijini.”
Kampeni hii inachanganya shughuli za moja kwa moja na ushiriki wa vyombo vya habari kufikia jamii kote Tanzania. Hizi ni pamoja na warsha za mafundi, ziara za gereji, mafunzo, na shughuli za kijamii katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Mwanza, Mbeya, na zaidi.
Dkt. Aileen Meena, Mkuu wa Masoko, Mawasiliano na Miradi ya Jamii wa Vivo Energy Tanzania, alisisitiza upande wa kijamii wa kampeni hiyo:
“Tukijenga juu ya mafanikio ya kampeni ya mwaka jana ya ‘Sheli Tumerudi Kivingine,’ kampeni ya leo ya ‘Uliza Oili ya Shell’ ni zaidi ya juhudi za kibiashara – ni harakati ya kubadili tabia, kuboresha huduma za injini, na kuimarisha maisha ya jamii. Kupitia kuendeleza ujuzi kwa kizazi kijacho na kuongeza uelewa, tunaunda thamani ya pamoja na kuimarisha nafasi ya Vivo Energy kama kinara katika ujumuishaji wa vijana, ushirikiano wa kijamii, na uendelevu.”
Akizungumza katika hafla hiyo, Mdillah Osward Mratibu wa Kozi fupi na uzalishaji, alisema:
“Tunathamini sana utekelezaji wa haraka na wa kujitolea wa Vivo Energy Tanzania kufuatia Mkataba wa Makubaliano, unaoonesha ushirikiano wa kweli zaidi ya makubaliano ya karatasi. Vivo Energy inachangia kwa kiasi kikubwa kutoa mafunzo ya vitendo yanayoendana na mahitaji ya soko la ajira la sasa.”
Kupitia kampeni ya “Uliza Oili ya Shell,” Vivo Energy Tanzania inathibitisha tena nafasi yake kama kampuni ya nishati inayoaminika na yenye maono ikichochea maendeleo, ikilinda injini, na kuwawezesha watu na jamii.