Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde, akiwa pamoja na Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Dkt. Janet Lekashingo, walipata fursa ya kutembelea banda la Puma Energy Tanzania, ambapo kampuni iliwakilishwa na Meneja Mauzo wake, Bw. Prosper Kasengela na kupata maelezo na ufahamu zaidi kuhusu mchango wao katika kukuza sekta hiyo muhimu.
Kongamano hilo limeonesha dhahiri umuhimu wa wadau wa nishati kama vile Puma Energy Tanzania katika kuhakikisha sekta ya madini inakua kwa kasi, kwa usalama na kwa tija. Kampuni hiyo imesisitiza kuwa itaendelea kushirikiana na wachimbaji wakubwa na wadogo nchini katika kuwapatia suluhisho bora za nishati ili kuchangia maendeleo ya kiuchumi ya taifa.
Puma Energy Tanzania inaendelea kuwa mdau muhimu katika kuchochea maendeleo ya sekta mbalimbali nchini zikiwemo madini, usafirishaji, ujenzi na usafiri wa anga, kwa kuzingatia ubora, usalama na kuwawezesha Watanzania katika shughuli za kijamii na kiuchumi.
Kampuni pia ilifanikiwa kutunikiwa tuzo maalum kwa kutambuliwa kwake kuunga mkono kongamano hilo.