Ruhuwiko-Songea.
Diwani wa Kata ya Ruhuwiko Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma Wilbert Mahundi, amesema hakuna diwani anaeweza kumaliza kero au changamoto zote za kata kwa wakati mmoja isipokuwa kwa awamu tofauti tofauti kulingana na vipaumbele na bajeti husika.
Akisoma utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia 2020-2025 mbele ya wanachama na wananchi wa Kata hiyo leo Juni 19, 2025, amesema kwa kiasi kikubwa huduma mbalimbali muhimu za kijamii zimewafikia wananchi.
Katika uongozi wake kwenye Sekta ya afya wamefanikiwa kujenga kituo cha afya cha Kata na kimekamilika pamoja na kutenga eneo Kilagano la hekari 20 kwaajili ya kuzikia.
Kadharika wamejenga shule mpya ya msingi Mapinduzi mtaa wa Ruhuwiko C, madarasa matano Shule la msingi Ruhuwiko, shule mpya ya sekondari ya kata Jumbe Idd inayopatikana eneo la Namanditi, pamoja na matundu ya vyoo kwenye shule nne za msingi ambazo ni Ruhuwiko, Huduma na Namanditi.
Kwa upande wa miundombinu, barabara mpya za mitaa Kilimota 11.7, ambapo Ruhuwiko kanisani, barabara 6, Ruhuwiko shuleni 7, Ruhuwiko C, barabara 5 na Namanditi barabara 7, stendi ya mabasi Ruhuwiko kutoka mjini, daraja jipya la Luwawasi, vivuko Ruhuwiko Shuleni na Kwa Kunja kanisani.
Amesema changamoto mbalimbali kama vile huduma ya umeme na maji vimeimarika zaidi ukilinganisha na awali huku eneo la utawala likiimarishwa zaidi kwa ujenzi wa ofisi mpya ya Kata ya Ruhuwiko, Ofisi mpya mtaa wa kanisani, kuanzisha kwa ujenzi wa ofisi ya mtaa wa Namanditi, ujenzi wa ofisi za mitaa ya Ruhuwiko shuleni na Ruhuwiko C.
Amewahimiza wananchi kukaa na kutafakari mafanikio hayo makubwa aliyoyafanya katika kipindi cha miaka mitano iliyopita kwani anania njema yakuhakikisha kata hiyo inazidi kupata maendeleo zaidi.