Tunayo furaha kutangaza kukamilika kwa uhamishaji wa biashara ya huduma za kibenki kwa wateja wa Hali ya juu na wa kawaida (rejareja) ya Standard Chartered kwa Access Bank PLC. Uhamisho huu ni sehemu ya mkakati wa kimataifa wa Standard Chartered, unaolenga kuongeza ufanisi wa uendeshaji, kupunguza ugumu, na kuongeza uwezo wa kutoa huduma kwa kiwango kikubwa.
Mnamo Aprili 2022, Standard Chartered ilifanya uamuzi wa kimkakati kujiondoa katika baadhi ya masoko, ikiwa ni pamoja na uamuzi wa kuacha kutoa huduma za benki ya watu binafsi na huduma kwa watu wa Hali ya juu (utajiri) nchini Tanzania. Uhamiaji huu wa leo kwenda Access Bank PLC unathibitisha kukamilika kwa mchakato huo wa kujiondoa, na kufungua ukurasa mpya kwa Access Bank PLC.
Herman Kasekende, Mkurugenzi Mtendaji wa Standard Chartered Tanzania, alisema, “Mabadiliko haya ni hatua muhimu kwa Standard Chartered tunapojielekeza upya katika maeneo yetu ya msingi ya kiutendaji. Kipaumbele chetu katika mchakato huu kimekuwa kuhakikisha mabadiliko haya yanakwenda vizuri kwa wafanyakazi na wateja wetu, ambao ndio msingi wa kila tunachofanya. Tuna imani kuwa chini ya Access Bank PLC, wateja wetu wa benki ya rejareja pamoja na wafanyakazi wataendelea kupata huduma na msaada wa kiwango cha juu kama walivyozoea.”
Licha ya kujiondoa katika sekta ya huduma za rejareja, Standard Chartered itaendelea kujitolea kwa Tanzania na itaendelea kuwa na uwepo imara, ikiweka mkazo kwenye biashara ya Benki kwa Makampuni na Uwekezaji (Corporate and Investment Banking) nchini.
Benki hii bado ni sehemu muhimu ya mpango wa kimkakati wa Standard Chartered Group barani Afrika. Standard Chartered imekuwa ikifanya kazi nchini Tanzania tangu mwaka 1917 na inaendelea kuwa mshirika muhimu kwa Makampuni, Taasisi, na Serikali.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Chartered (T) Bw. Herman Kasekende (kulia) na Imani John (kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Access Bank, Wakisaini mkataba wa kukabidhiwa kwa biashara za kibenki kwa wateja wa hali ya juu na reja reja ya Standard Chartered kwa Access Bank PLC jijini Dar es Salaam