Makamu Mkuu wa Chuo cha Mtakatifu Augustino(SAUT) Mwanza anayeshughulikia Taaluma Prof. Hosea Rwegoshora, akizungumza na wanafunzi wa vyuo mbalimbali vya mkoa wa Mwanza kwenye kongamano la kuwajengea uwezo, kuzitambua fursa na kuzifanyia kazi lililoandaliwa na AIESEC na kudhaminiwa na Barrick.
Makamu Mkuu wa Chuo cha Mtakatifu Augustino(SAUT) Mwanza anayeshughulikia Taaluma Prof. Hosea Rwegoshora, akizungumza na wanafunzi wa vyuo mbalimbali vya mkoa wa Mwanza kwenye kongamano la kuwajengea uwezo, kuzitambua fursa na kuzifanyia kazi lililoandaliwa na AIESEC na kudhaminiwa na Barrick.
Afisa Raslimali Watu Mwandamizi wa Barrick North Mara, Emmanuel Msacky akiongea na wanafunzi wakati wa kongamano hilo
Wanafunzi wakifuatilia mada mbalimbali
Wanafunzi wakifuatilia mada mbalimbali
Wafanyakazi wa Barrick katika picha ya pamoja na meza kuu
Vijana wasomi nchini waliopo vyuoni wametakiwa kuongeza bidii, maarifa katika masomo yao na kuwa wabunifu ili kuweza kupenya kwenye soko la ajira kwenye taasisi mbalimbali ikiwemo migodini sambamba na kuweza kujiajiri kwa kutumia taaluma zao pindi wamalizapo masomo sambamba na kuchangamkia fursa muhimu kwa mafanikio ya kitaaluma.
Ushauri huo umetolewa na , Makamu Mkuu wa Chuo cha Mtakatifu Augustino (SAUT),Profesa Hosea Rwegoshora, wakati wa kongamano la Wanafunzi wa vyuo vikuu vilivyopo mkoani Mwanza lililoandaliwa na taasisi ya kuchipua na kuendeleza vipaji kwa vijana ya AIESEC Tanzania ambalo limedhaminiwa na Barrick nchini kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali ambalo limefanyika katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino kilichopo jijini Mwanza.
Amesema kuwa hivi sasa tuko kwenye kipindi cha mapinduzi makubwa sayansi na teknolojia hivyo aliwaasa wanafunzi kusoma kwa bidii ili kuweza kuingia soko la ushindani wa ajira hapa nchini sambamba na kuibua fursa za kujiajiri.
Naye Afisa Raslimali Watu Mwandamizi kutoka Barrick North Mara, Emmanuel Msacky , wakati akieleza shughuli za kampuni na programu zake wezeshi kwa jamii kwa washiriki, alisema kampuni ya Barrick nchini ambayo inaendesha shughuli zake kwa ubia na Serikali ya Tanzania kupitia kampuni ya Twiga Minerals, itaendelea kutafuta rasilimali watu kwa ajili ya kufanya kazi kwenye migodi yake ikiwemo vijana wanaohitimu kutoka kwenye vyuo vikuu mbalimbali na vya ufundi vya kati hapa nchini na lengo kubwa kuhakikisha inaendelea kuibua vipaji na kuunga mkono jitihada za Serikali za kupunguza changamoto ya ukosefu wa ajira.
Bw. Msacky , aliwaeleza washiriki kuwa migodi inayomilikiwa na Barrick nchini ya North Mara na Bulyanhulu imekuwa ikitoa fursa kwa vijana wa vyuo vikuu kuomba ajira mara tu wanapomaliza masomo na wakiwa kazini wanapata nafasi ya kujengewa uwezo na kampuni pia kampuni inayo programu ya kutoa nafasi ya mafunzo kwa vitendo kwa Wanafunzi wanapokuwa bado wako vyuoni.
Semina za kuwanoa vijana wasomi vyuoni kupitia taasisi ya AIESEC kwa udhamini wa Barrick nchini mwaka huu tayari zimefanyika katika mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Dodoma, Arusha, Iringa na Zanzibar.