Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (LST) imeshiriki kutoa huduma ya msaada wa kisheria kwenye Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia iliyofanyika mkoani Dar es Salaam kuanzia tarehe 16-25 Juni, 2025.
Kampeni hiyo ilizinduliwa rasmi tarehe 16 Juni, 2025 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa katika viwanja vya Maturubai, Mbagala jijini Dar es Salaam.
Kaulimbiu ya kampeni hiyo ni “msaada wa kisheria kwa haki, usawa, amani na maendeleo”.
Sambamba na kampeni hiyo, LST kupitia kituo chake cha kutoa msaada wa kisheria (LST Legal Aid Centre) inaendelea kutoa huduma hizo bure kwa wahitaji mbalimbali katika ofisi za Taasisi hiyo zilizopo maeneo ya Sinza jijini Dar es Salaam.