WADAU wa Sekta ya Afya ya Uzazi Wameiomba Serikali kutoa Kodi katika Kifaa tiba hasa Taulo za kike Kwa Wanawake na Mabinti ili ziweze kuwafikia kwa wingi na Kupata Hedhi iliyo salama kwa kumudu gharama za taulo hizo.
Akizungumza na Wanahabari Katika Hafla ya Uzinduzi wa Taulo za Kike aina ya Rayan sanitary pads ,Mkurugenzi wa Binti Salha Foundation Salha Aziz amesema kuna changamoto mbalimbali ambazo zimekuwa zikiwakumba Wanawake na Mabinti wadogo wakiwa katika siku zao za Hedhi hasa kukosekana na kifaa tiba hicho.
“Kumekuwepo changamoto mbalimbali inayosababisha Kutopatikana Kwa Hedhi isiyo salama kutokana na kutofikiwa na kutomudu gharama za kupata taulo za Kike na Kulazimika kutumia vitu hatarishi ikiwemo Kiporo cha Ugali,Magodoro ,Vipande vya Kanga visivyo na usafi unaohitajika.”
Hata hivyo Aziz ameongeza kuwa Wadau wa Sekta ya Afya ya Uzazi na Hedhi Salama Kwa taasisi na Mashirika yasiyo ya Kiserikali yataendelea kupaza sauti kwa Serikali Kuhakikisha Wanatoa tozo katika Taulo za Kike ili Mabinti Mashuleni wapate taulo hizo kwa wakati.
Kwa upande Wake Daktari kutoka Hospitali ya Muhimbili Genieveve Felix amesema Jamii imekuwa ikikumbana na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa Elimu kwa Mabinti wadogo namna sahihi ya kujikinga wakati wa hedhi na bidhaa ipi ni salama zaidi.
Pia amesema mbali na changamoto hizo ,ipo changamoto kubwa ya bei za taulo za kike kutokuwa rafiki kwa watumiaji hususani kwa Wasichana Mashuleni.
Hata hivyo Mmoja ya Washiriki katika Uzinduzi huo wa Taulo za Kike aina ya Rayan Othman Juma Kutoka shirika la Ecao amesema Jamii inapaswa kumsaidia binti ambae yupo katika hedhi pamoja huku Wanaume Kuwahakikisha Wanawake Wanapata Hedhi salama kama sehemu ya ratiba zao kwa kila mwezi.