Kada wa Chama Cha Mapinduzi CCM, Abuubakari Ally ( Boka) amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa kugombea nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Kigamboni, Dar es Salaam.
Abuubakari, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Dar es salaam, amefika katika ofisi za Chama wilayani humo leo na kukabidhiwa fomu na Katibu wa CCM wa wilaya hiyo, stanley Mkandawile.
Pamoja na kujihusisha na Siasa Boka ni mdau wa masuala ya afya na michezo nchini.
Wengine waliochukua fomu katika jimbo hilo ni Ally Mandai, Rais wa Yanga Mhandisi Hersi Said, Dokta Henjewele,Diwani wa Kata ya Msasani Luca Nighest.