Aliyekuwa Diwani wa Msasani na mfanyabiashara maarufu, Bw Luca Hakim Neghesti, amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kuwania Ubunge wa Jimbo la Kigamboni.
Bw Neghest ni mjasiriamali mwenye mafanikio, mwanzilishi wa taasisi mbalimbali zikiwemo Bongo5 Media na amekuwa na mchango mkubwa katika masuala ya maendeleo katika Kata ya Msasani.
Bw Neghest ambaye ni mume wa Miss Tanzania wa mwaka 2005, Nancy Sumari ambaye aliitoa kimasomaso Tanzania kwa kushinda taji la Miss World Africa pia ana uzoefu mkubwa katika utumishi wa umma pamoja na sekta binafsi.
Diwani wa zamani wa Kata ya Msasani, Bw Luca Neghesti (kulia) akipokea fomu kutoka kwa Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM) wa Wilaya ya Kigamboni, Stanley Mkandawile kuwania Ubunge wa Jimbo la Kigamboni.
Diwani wa zamani wa Kata ya Msasani, Bw Luca Neghesti (kulia) akipozi na mkewe, Miss Tanzania 2005 na Miss World Africa, Nancy Sumari mara baada ya kuchukua fomu ya maombi ya kuwania Ubunge wa Jimbo la Kigamboni kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).