KADA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jerry Silaa, amechukua na kisha kurejesha fomu baada ya kuijaza ya kuomba ridhaa ya Chama kuwania ubunge katika Jimbo la Ukonga jijini Dar es Salaam.
Silaa, alichukua na kurejesha fomu hiyo katika Ofisi ya CCM Wilaya ya Ilala ambapo alikabidhiwa na Katibu wa Chama wa wilaya hiyo Sylivester Yared, mapema leo.
Silaa anaomba ridhaa ya Chama kutetea kiti cha Ubunge wa Jimbo la Ukonga na ambapo hadi kufikia saa nane mchana hakukuwa na kada mwingine aliyejitokeza kuchukua fomu ya kuomba ridhaa katika jimbo hilo.