![]() |
Mtia nia James Innocent Mkinga (kulia), Mtaalamu mbobezi katika Fani ya Teknojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) akichukua fomu yake kuomba kuteuliwa kugombea jimbo hilo. |
JOTO la Siasa katika Jimbo la Uchaguzi la Ludewa limezidi kupanda
kufuatia kuendelea kujitokeza kwa watia nia mbalimbali wanaoashiria kuwepo kwa
mchuano mkali jimboni humo.
Jumapili Juni 29 2025, Mtia nia James Innocent Mkinga, Mtaalamu
mbobezi katika Fani ya Teknojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), Kada CCM na
mwana harakati wa Maendeleo ya Vijana amejitokeza kwa mara ya pili kuchukua
Fomu ili kushiriki katika mchakato wa kupata nafasi ya kupeperusha bendera ya
Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi wa Mbunge wa Jimbo hilo.