Aliyekuwa Mbubge wa Viti maalum kwa kipindi cha mwaka 2020/2025 kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi (CCM) Hawa Mchafu Chakoma amejitosa kuchukua fomu kwa kwa ajili ya kutetea nafasi yake ya Ubunge kwa kipindi cha mwaka 2025/2030.
Mchafu ,amechukua fomu hiyo katika ofisi ya Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania ( UWT)iliyopo katika jengo la Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani Kibaha Mjini.
Mchafu amebainisha kwamba lengo lake kubwa ni kuhakikisha anaendelea kushirikiana na wananchi mbali mbali katika suala zima la kuchochea kasi ya maendeleo.
Aidha ,Mchafu ambaye ni mkongwe wa Siasa hapa nchini amechukua fomu kwa ajili ya kutaka kuendelea kusaidia jamii hususani katika kutatua changamoto za Wanawake wa Mkoa wa Pwani.
Hata hivyo,Mchafu katika kipindi cha miaka mitano iliyopita amefanya mambo makubwa katika jamii na kwamba anataka kuendelea kufanya mengi zaidi katika kipindi kijacho.