Wachezaji wa timu ya Ng’wasabuka na Busindi wakiwania Mpira wakati Mechi ikiendelea

*
Timu za soka za Kakola FC na Ng’wasabuka FC, zimefanikiwa kuingia katika ngazi ya fainali ya michuano ya Mahusiano Sports Bonanza 2025 iliyoandaliwa na mgodi wa Barrick Bulyanhulu uliopo katika halmashauri ya Msalala mkoani Shinyanga.
Hatua hii inakuja, baada ya timu ya Kakola kutoka Kata ya Bulyanhulu, kuifunga Buyange mabao 2-0 katika mechi ya nusu fainali ambapo timu ya Ng’wasabuka iliifunga timu ya Busindi mabao 3-1.
Mechi ya fainali ambayo inatarajia kuwa na msisimko mkubwa katika maeneo ya vitongoji vunavyozunguka mgodi wa Bulyanhulu itafanyika Ijumaa ya Julai 4, katika uwanja wa Shule ya Msingi Kakola ambapo timu iliyoshinda itapatiwa zawadi kutoka Barrick Bulyanhulu pia timu zilizoshiriki zitapatiwazawadi mbalimbali.
Michuano hii ya soka ya Mahusiano Sports Bonanza yameshirikisha timu 16 za vijana kutoka vijiji 16 kutoka kata 3 za Bugarama,Bulyanhulu na Mwingiro.
Akiongea wakati wa uzinduzi wa mashindano haya,Meneja Mkuu wa Barrick Bulyanhulu,Johan Labuschagne alisema mgodi utaendelea kuunga mkono jitihada za Serikali za kukuza michezo na kuibua vipaji,sambamba na kudumisha uhusiano na jamii inayozunguka mgodi kupitia jukwaa hili la michezo.
Wakazi wa kata hizo ambao kwa kipindi cha mwezi mzima walikuwa wakishuhudia burudani za mashindano haya wameupongeza mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa kuanzisha na kuyafadhili na kueleza kuwa kuwa mbali na kuleta burudani na kuwaunganisha vijana pia michezo inasaidia kujenga afya sambamba na kuwaepusha kujihusisha na vitendo viovu katika jamii.