RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amewaapisha Mkuu wa Mkoa na Wakuu wa Wilaya aliowateua hivi karibuni.
Hafla hiyo imefanyika leo, tarehe 3 Julai 2025,Ikulu ya Zanzibar.
Walioapishwa ni:
1. MHE. HAMIDA MUSSA KHAMIS, KUWA MKUU WA MKOA KUSINI UNGUJA.
2. MHE. CASSIAN GALLOS NYIMBO, KUWA MKUU WA WILAYA MAGHARIBI A UNGUJA
3. MHE. RAJAB ALI RAJAB, KUWA MKUU WA WILAYA YA KATI UNGUJA
4. MHE. MIZA HASSAN FAKI, KUWA MKUU WA WILAYA MKOANI, PEMBA
5. MHE. MOHAMED ALI ABDALLAH KUWA MKUU WA WILAYA MJINI, UNGUJA
6. MHE. AMOUR YUSSUF MMANGA KUWA MKUU WA WILAYA MAGHARIBI B, UNGUJA.
Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, vikosi vya Ulinzi na Usalama, pamoja na viongozi wa dini, wakiongozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla.