Na Said Mwishehe,Michuzi TV
MAMLAKA ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA)imewakaribisha wananchi wanaofika katika Maonesho ya Biashara ya 49 ya Kimataita yanayoendelea Sabasaba jijini Dar es Salaam kufika katika banda lao ili kupata uelewa wa masuala yanayohusu uwekezaji katika masoko ya mitaji.
Akizungumza leo na waandishi wa habari katika Banda la CMSA lililopo katika Jengo la Wizara ya Fedha katika maonesho hayo yanayoendelea Sabasaba Stella Anastaz ambaye ni Ofisa Uhusiano na Elimu kwa Umma amesema katika
Maonesho kwa lengo la kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu masoko ya mitaji.
“CMSA ni mamlaka ya serikali iliyo chini ya Wizara ya Fedha na Uchumi iliyoanzishwa na Sheria namba. 5 ya Masoko ya … tuko katika msimu huu wa 49 wa maonesho ya kimataifa ya biashara Dar es Salaam na tuko hapa pamoja na watalaam wetu wote wa makoso ambao wanashiriki kwa namna moja au nyingine kuwasaidia wawekezaji ambao ni kampuni au mmoja mmoja …
“Kwahiyo napenda kuchukua fursa hii kuwakaribisha wananchi ambao wanapata nafasi ya kuja Sabasaba wasikose kupita banda la CMSA ili waweze kukutana na watalaam wa masoko waliobobea katika nyanja mbalimbali za soko ikiwemo uwekezaji katika hisa , uwekezaji kwenye vipande pamoja na uwekezaji katika hati fungani.
“Wananchi watakaofika hapa wanaweza kupata ufahamu wa masuala mbalimbali yanayohusu masoko ya mitaji pamoja na kuulizwa maswali na kujibiwa. .. ndio maana tunawaarifu wananchi waje CMSA kwasababu hapa tumekuja na watalaam wote wa soko.
Amefafanua kuwa watalaam wa masoko wanaotoa elimu na kujibu maswali ya wananchi ni wamebobezi na wamepewa leseni na mamlaka hiyo baada ya kuhitimu kozi maalum ambayo inaendeshwa na mamlaka.
Hivyo ni watalamu hao kazi yao kubwa ni kutoa ushauri wa wapi uende kuwekeza baada ya kumsikiliza muwekezaji na kujua huyu ni nwekezaji wa namna gani kwasababu kwenye upande wa masoko ya mitaji huo ni uwekezaji wa muda mrefu .
“Kwahiyo akija mtu ambaye anategemea labda aweke leo na baada ya siku mbili tatu atoke inaweza kumletea ukakasi lakini kwa muwekezaji ambaye ana plani ya muda mrefu akifika hapa ataweza kueleweshwa zaidi …
“Atapewa hali ya soko ikoje kutokana na Kampuni mbalimbali ambazo zimeorodheshwa sokoni au kama anataka uwekezaji wa pamoja atakutana na watalaam wa uwekezaji wa pamoja watamshauri ni wapi aende kwasababu gani, Kwahiyo tumekuja na hawa watalaam kwasababu hiyo zaidi.”
Wakati huo huo amewaalika wanafunzi ambao wako kwenye vyuo vikuu pamoja na vyuo vingine vya elimu ya juu kufika katika banda la CMSA kwasababu Julai mpaka Agosti mwaka huu wanaprogramu ya shindano la wanafunzi wa elimu ya juu ,ambapo shindano hilo lina lengo la kutoa elimu ya masoko ya mitaji kwa vijana katika sekta ya elimu
“Kwahiyo wakifika hapa waje tuwaeleweshe ni jinsi gani watajisajili na hatimaye kuweza kufanya challenge hiyo.Kwa ambao hataweza kufika wakitembelea tovuti ya mamlaka ambayo ni www.cmsa .co. tz wataweza kukutana na taarifa za ni namna gani wanaweza kujiunga kwenye shindano hili ambapo wakijiunga kwenye shindano hili zawadi mbalimbali zitatolewa .
“Zawadi za fedha pamoja na kutembelea masoko ya mitaji kuona ni namna gani masoko ya mitaji yanafanya kazi na namna gani cmsa inasimamia uwekezaji kwenye masoko ya mitaji,”amesema Anastazi.
Kuhusu usalama wa masoko ya mitaji amesema ni salama kabisa pia ni aina sahihi kabisa ya uwekezaji,kama inavyoeleweka CMSA ni mkono wa Serikali ambao unasimimamia utimilifu wa uwekezaji huo ikiwa pamoja na kuangalia uwino kati ya wakala wa soko , soko lenyewe na wawekezaji.