NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV
Bodi ya Bima ya Amana (DIB) inaendelea kutoa elimu kwa wananchi na wadau mbalimbali katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama SABASABA, yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Barabara ya Nyerere, Jijini Dar es Salaam.
Wananchi wote wanakaribishwa kutembelea banda la DIB ili kupata elimu kuhusu majukumu ya Bodi, umuhimu wa ulinzi wa amana zao kwenye taasisi za fedha, pamoja na nafasi ya DIB katika kuhakikisha usalama na uthabiti wa mfumo wa fedha nchini.
Kwa sasa, DIB ipo katika mchakato wa kuboresha muundo wake wa kisheria na kiutendaji, hatua inayolenga kuimarisha mchango wake katika sekta ya fedha na kuhakikisha inajitegemea kwa ufanisi zaidi.
Mabadiliko haya yanatarajiwa kuongeza ufanisi wa DIB katika kutekeleza majukumu yake ya msingi, ikiwemo kulinda haki za wateja wa taasisi za fedha na kuimarisha imani ya wananchi katika mfumo wa kifedha wa Tanzania.