Mkuu wa Kanda ya Kaskazini, Vodacom Tanzania PLC, George Venanty (kushoto) akimkabidhi kiti cha ulemavu mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Msingi Mkata ambapo pia walikabidhi matundu ya choo 10, magodoro 40, vitanda 20, na viti vya walemavu 47 kwa shule hiyo ikiwa ni sehemu ya shughuli zinazofanywa katika Msafara wa Twende Butiama ambao umeanza Julai 3, 2025.
Pia msafara huu, chini ya ufadhili wa Vodacom Tanzania na Benki ya Stanbic Tanzania, walifanikiwa kupanda jumla ya miti 100 katika kata ya Mkata iliyopo katika wilaya ya Handeni Vijijini, mkoani Tanga.