Mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa Shahada ya Awali ya Sayansi katika Mifumo ya Habari za Afya ( HIS) kutoka Shule Kuu ya Uuguzi na Afya ya Jamii (SoNPH) Bw. Lucas Allen Haule ameibuka Mshindi wa Kwanza wa bunifu ya Utengenezaji wa Nembo ya Made in Tanzania ambapo lilihusisha zaidi ya washiriki 80 nchini Tanzania.... Read More
Mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa Shahada ya Awali ya Sayansi katika Mifumo ya Habari za Afya ( HIS) kutoka Shule Kuu ya Uuguzi na Afya ya Jamii (SoNPH) Bw. Lucas Allen Haule ameibuka Mshindi wa Kwanza wa bunifu ya Utengenezaji wa Nembo ya Made in Tanzania ambapo lilihusisha zaidi ya washiriki 80 nchini Tanzania.
Shindano hilo lililaratibiwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania ( TANTRADE) na leo tarehe 8 Julai katika Ukumbi wa Karume “Sabasaba” amekabidhiwa zawadi ya Ushindi na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe ( Mb).
Aidha; Nembo hiyo ilizunduliwa Rasmi tarehe 7 Julai, 2025 na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Mwinyi wakati wa Ufunguzi wa Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba).