
“Ni hatua muhimu katika kuhakikisha huduma ya umeme inaimarishwa ili kuendana na kasi ya maendeleo,” amesema Mpogolo.
Aidha, Mkuu huyo wa Wilaya alitumia fursa hiyo kupeleka salamu za shukrani kwa Mheshimiwa Rais kwa kushughulikia kwa vitendo changamoto ya maji jijini Dar es Salaam.
“Tupelekee salamu kwa Mheshimiwa Rais kwa kuleta zaidi ya Shilingi bilioni 37 ambazo zimewezesha ujenzi wa tanki kubwa la maji lililopo Bangulo, Wilaya ya Ilala. Tenki hilo litakuwa sehemu muhimu ya kusaidia upatikanaji wa maji kwa wakazi wa jiji na pia litachangia katika upatikanaji wa umeme,” ameongeza.
Vilevile, ameeleza shukrani kwa Serikali kwa kuendelea kupeleka fedha za maendeleo katika wilaya mbalimbali za Dar es Salaam, jambo ambalo limechochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi na kuchangia ustawi wa nchi kwa ujumla.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko (wa tatu kulia) akikagua maendeleo ya miradi ya kuzalisha umeme kwa gesi asilia katika vituo vya Kinyerezi I, Kinyerezi I Extension na Kinyerezi II leo, Julai 10, 2025, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Lazaro Twange akisalimiana na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Mashaka Biteko wakati akiwasili katika miradi ya kuzalisha umeme leo, Julai 10, 2025, jijini Dar es Salaam.

Mitambo ya miradi ya kuzalisha umeme kwa gesi asilia katika vituo vya Kinyerezi I, Kinyerezi I Extension na Kinyerezi II.










