Waziri wa maji Mh.Jumaa Aweso (Mb) amewatoa hofu wakazi wa mikoa ya Dar na Pwani kuhusu upatikanaji wa huduma ya majisafi mara baada ya kutembelea na kukagua maboresho yaliyofanyika katika mtambo wa kuzalisha maji Ruvu juu
“Kwakweli hali inaridhisha sasa, nilitoa maagizo ya maboresho katika mtambo huu, leo nimekuja kujionea, nitoe pongeze kwa Menejimenti ya DAWASA kazi kubwa imefanyika hapa na katika chanzo tumekuta maji ya kutosha kabisa” ameeleza Mh.Aweso
Aweso ameongeza kwakutoa maelekezo kwa DAWASA kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji bila kikwazo chochote kwani hali ya mtambo ni nzuri na maji yapo yakutosha.
“Maji haya sasa ni wajibu wa DAWASA kuhakikisha yanawafikia wananchi na kunufaika nayo, Wizara itaendelea kuwapa ushirikiano kuhakikisha hamkwami, lakini pia ili kuboresha huduma Serikali imeasha agiza pampu mpya katika mtambo huu ili ziwe mbadala pale kunapotokea hitilafu” amesema Aweso.
Mh.Aweso amemaliza kwa kuishukuri Serikali ya mkoa wa Pwani pamoja na Chama Cha Cha mapinduzi kwa ushirikiano wa kutosha kwa Wizara hali inayofanya huduma ya maji kuwa ya uhakika.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya maji, Mhandisi Mwajuma Waziri ameipongeza DAWASA Kwa maboresho makubwa waliyofanya na kuwataka kuhakikisha wanawasikilza wananchi ili kuondoa malalamiko huku wakihakiksha wanapambana na upotevu wa maji kwa kudhibiti mivujo.
Nae Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Mh.Nickson Simon ameeleza kuwa wanashirikiana kwa karibu na DAWASA na Bonde Wami-Ruvu katika utafutaji wa vyanzo mbadala vitakavyosaidia kuzuia uharibifu katika chanzo Cha mto Ruvu ikiwemo ujenzi wa birika za kunyweshea mifugo katika vijiji vya Minazi Mikinda na Mpera-mumbi.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Mkama Bwire ameeleza kuwa kwa mwaka huu wa fedha 2025 – 2026 Mamlaka imewekeza nguvu kubwa katika kuwaungia wananchi huduma ya maji ambapo imelenga kuunganisha wateja wapya 72,000.