Na MWANDISHI WETU
BENDI ya muziki wa dansi ya The Arican Stars Internatiobal ‘Twanga Pepeta’ inatarajia kufanya onesho kubwa na la aina yake katika Ukumbi wa New Wallet Pub, uliopo Kwa Rais, Kata ya Pugu, Ilala, jijini Dar es Salaam.
Onesho hilo linatarajiwa kufanyika Julai 19 mwaka huu na litakuwa halina kiingilio.
Akizungumza na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam, Mwandaaji wa onesho hilo, Emmanuel Tengia, amesema, onesho hilo la Twanga Pepeta ni mwanzo tu wa mfurulizo wa burudani katika ukumbi huo na Kata ya Pugu.
“Tulianza na bendi ya Msondo, awamu hii tunashusha kikosi kizima cha Twanga Pepeta. Onesho litakuwa kubwa na tumejipanga vyema kuhakikisha mashabiki watakao ingia ukumbini wanakata kiu,”amesema Tengia.
Ameeleza, hakuta kuwa na kiingilia kwa mashabiki na watatakiwa kununua kinywaji au chochote ukumbini.
Tengia, ameeleza dhamira ni kuhakikisha wananchi wa Kata ya Pugu na viunga vyake wanapata eneo la burudani na starehe.
“Kata ya Pugu hakukuwa na eneo maalumu ambalo wananchi wanaweza kupata burudani za bendi kubwa hapa nchini. New Wallet tumeamua kuwasogezea burudani hiyo. Baada ya Twanga Pepeta bendi itakayofuata ni FM Academia.”ameeleza.