Wafanyakazi wawili wa mamlaka ya mapato Tanzania mkoa wa Mwanza TRA wamefariki papo hapo baada ya kupata ajali ya gari.
Akitoa taarifa ya ajali hiyo kamanda wa polisi mkoa wa Geita SACP Safia Jongo amesema kuwa ajali hiyo ilitokea mnamo July 20 majira ya saa 10 alfajiri katika eneo la bwawani mamlaka ya mji mdogo Katoro mkoani Geita ikitokea mkoani Kagera.
Chanzo cha ajali hiyo kimetajwa kuwa ni uchovu wa dereva wa gari hiyo ambayo ni mali ya TRA ambaye alikuwa ameendesha kwa muda mrefu.
Ajali hiyo imesababisha vifo vya watu wawili ambao ni maafisa Forodha Emmanuel Leonard na Mwita John pamoja na majeruhi mmoja Julius Dismas ambaye ni dereva wa gari hiyo ambaye alisharuhusiwa hospitali
Jeshi la polisi mkoa wa Geita linatoa wito kwa madereva kuzingatia sheria za barabarani pamoja na kujipa muda wa kupumzika kabla hawajaanza safari ili kupunguza ajali za barabarani.