Na Mwandishi wetu Dodoma
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt Edwin Mhede amesema kuwa Serikali ilizalisha vipande vya ngozi Milioni 11.7 kwa mwaka 2020-2021 na kwa mwaka 2024-2025 imezalisha vipande Milioni 15.2 huku kila mwaka kukiwa na ongezeko lakini lengo la Serikali ni kwenda zaidi ya hapo hiyo Milioni 15.2 katika uzalishaji.
Dkt Mhede ameyazungumza hayo leo Jijini Dodoma Julai 23,2025 wakati akifungua Kongamano la Wadau wa Sekta ya Mifugo la Mjadala wa Ngazi ya juu kuhusu kufungua fursa za Minyororo ya Thamani ya Mifugo na Ngozi Nchini Tanzania lililoratibiwa na Benki ya Equity.
Ambapo pia ameongeza kuwa hadi jana Serikali chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi wamechanja na kutambua Mifugo ipatayo Milioni 16 ambayo zoezi lake lilianza huko Mkoani Simiyu na kukusudia kumalizika kabla ya Octoba kwa awamu hii ya kwanza,lakini kuendelea katika kipindi cha miaka 5 ili kuhakikisha mifugo yote Nchini imepata chanjo na kutambauliwa kwani kwa kufanya hivyo kwa kudhibiti magonjwa kunaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa kupatikana kwa ngozi nzuri na zenye ubora.
“Kwa upande wa ngozi mwaka 2020-2021 tulizalisha vipande Milioni 11.7 wakati kwa mwaka 2024-2025 tumezalisha vipande Milioni 15.2 na hapo kumekuwa na ongezeko la kila mwaka na niatarajio ya Serikali kwenda zaidi ya hiyo Milioni 15.2 katika uzalishaji”.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu Benki ya Equity Bi Isabela Maganga amesema kuwa wanatambua jitihada kubwa iliyowekwa na Serikali katika Sekta ya mifugo kuhakikisha kwamba wanainyanyua Sekta hiyo ya mifugo Nchini Tanzania.
Lakini wao kama Bank wanaona kuwa Sekta ya mifugo ni eneo ambalo wanahitaji kuwa wadau wakubwa katika masuala ya kifedha na elimu ya fedha katika kukuza thamani ya Sekta hiyo hususani ni katika kufungua fursa iliyopo katika zao la ngozi.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Equity Benki Dkt Florence Tuluka amesema kuwa lengo la Benki hiyo kuwakutanisha wadau hao ni kuona namna gani inaweza kusaidia kufanya mabadiliko katika sekta ya ngozi na kuona Sekta hiyo inaweza kuchangia zaidi katika Uchumi wa nchi ya Tanzania na kuleta manufaa zaidi.
Na kuongeza kuwa mifugo ina nafasi kubwa katika uchuni na kuajiri wananchi wengi lakini bado kuna umuhimi wa kuona namna inaweza kuchangia zaidi katika ustawi wa Watanzania wote na Sekta ya ngozi kupata nafasi ile inayotarajiwa ili ichangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya Nchi.
“Kama wote tunavyofahamu hapa Tanzania mifugo ina nafsi kubwa sana katika uchumi wetu na ina ajiri wananchi wengi sana hapa nchini Tanzania,lakini tunaona kuna umuhimu mkubwa bado wa kuona namna gani hii Sekta ya mifugo inaweza ikachangia zaidi katika ustawi wa Watanzania wote”.
Kongamano hili ni la siku moja na limerabiwa na Benki ya Equity na kujumuisha Wadau mbalimbali wa Sekta ya Mifugo kuangazia namna ya kupata fursa mbalimbali Duniani katika Sekta ndogo ya Ngozi.