
Jeshi la Uhamiaji mkoani Geita limewakamata jumla ya watu 54 raia wa kigeni kutoka nchi za Burundi, Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), kwa tuhuma za kuishi nchini kinyume cha sheria, bila kuwa na vibali halali vinavyowaruhusu kuendelea kuwepo ndani ya mipaka ya Tanzania.
Akizungumza na waandishi wa habari tarehe 22 Julai 2025, Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji Mkoa wa Geita, James Mwanjotile, amesema operesheni maalum inaendelea kufanyika kwa ajili ya kuwasaka wahamiaji haramu wanaoishi nchini kinyume cha sheria.
Kamishna Mwanjotile ametoa wito kwa wananchi kushirikiana na vyombo vya dola kwa kutoa taarifa kuhusu watu wanaoishi nchini bila vibali, akisisitiza kuwa ulinzi wa nchi ni jukumu la kila mmoja.