Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufani, Jacobs Mwambegele akizungumza wakati akifunga mafunzo ya siku tatu kwa watendaji wa uchaguzi mkuu kutoka mikoa ya Shinyanga na Simiyu leo Julai 23, 2025. Mafunzo hayo yamefanyika mkoani Shinyanga kuanzia Julai 21 hadi 23 mwaka huu. (Picha na INEC).

Mwenyekiti wa Mafunzo Ndg. Faustine Lagwen, akizungumza jambo.
Washiriki wakifuatilia ufungaji wa mafunzo hayo.
Washiriki kutoka mikoa ya Shinyanga na Simiyu wakifuatilia ufungaji wa mafunzo hayo.
Na. Mwandishi wetu.
Uchaguzi imewaelekeza watendaji wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 kufanya vikao na
viongozi wa vyama vya siasa kujadili masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na
kuhakikisha kuwa uteuzi wa wagombea unafanyika kwa mujibu wa sheria.
Maelekezo hayo yametolewa na
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs
Mwambegele wakati akifunga mafunzo kwa watendaji wa uchaguzi mkoani Shinyanga
leo Julai 23, 2025.
“Mtatakiwa kuyatafsiri mafunzo haya kwenye usimamizi wenu
wa shughuli za kila siku za masuala ya uchaguzi kwa kuanza na vikao na vyama
vya siasa, utoaji wa fomu za uteuzi na uteuzi wa wagombea wa nafasi za ubunge
na kuhakikisha utoaji wa fomu za uteuzi na uteuzi wenyewe ngazi ya udiwani
ufanyike kwa mujibu wa sheria,” amesema.
Amewaelekeza kuitisha na kuratibu kamati za upangaji wa ratiba za kampeni
na kuitisha kamati za maadili iwapo kuna changamoto zitajitokeza wakati wa kampeni.
Jaji Mwambegele
amewakumbusha watedaji hao kuhusu wajibu wao wa kutoa mafunzo kwa wasimamizi wa
uchaguzi ngazi ya vituo na kuratibu na kusimamia vizuri na kwa weledi uchaguzi
ngazi ya vituo.
“Mafunzo mtakayowapa yatawawezesha kuratibu na kusimamia
uchaguzi ngazi ya kata vizuri na kwa weledi. Hivyo, jukumu lenu ni kutoa
mafunzo sahihi, kwa kuonesha kwa vitendo yote wanavyotakiwa kuyafanya
wasimamizi wasaidizi ngazi ya Kata,” amesema.
Akifunga mafunzo kama hayo Kisiwani Pemba, Zanzibar, Makamu
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani (Mstaafu)
Mbarouk Salim Mbarouk amewakumbusha watendaji hao wajibu wao wa kubandika mabango, orodha ya majina ya wapiga kura na
matangazo au taarifa zinazopaswa kuwafikia wapiga kura kwa kuwa ni takwa la
kisheria na kanuni zinazosimamia uchaguzi.

“Ni wajibu wenu kuhakikisha mabango, matangazo, orodha ya majina ya wapiga
kura na taarifa yoyote inayotakiwa kubandikwa kulingana na kalenda ya
utekelezaji wa majukumu ya uchaguzi inabandikwa ili kuepusha malalamiko ya ukiukwaji
wa masharti ya sheria na kanuni za uchaguzi,” amesema.

Amewasisitiza watendaji hao kutoa taarifa mbalimbali kwenye vyombo vya
habari ili kuwajulisha wananchi na wadau mambo mbalimbali ya uchaguzi.
“Hakikisheni mnajiandaa kabla ya kukutana na vyombo vya habari. Pima
taarifa yako unayotaka kuitoa kabla hujaitoa ili kuepuka kuleta taharuki badala
ya utulivu katika eneo lako na Taifa kwa ujumla,” amesema.
Mafunzo hayo yamefanyika kwa
siku tatu kwenye mikoa mbalimbali nchini na yanawajumuisha waratibu wa
uchaguzi, wasimamizi wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya
jimbo.
Tume iliyagawa mafunzo hayo
kwenye awamu mbili ambapo awamu hii ya pili ilihusisha mikoa ya Simiyu,
Shinyanga, Kusini Pemba, Kaskazini Pemba, Mwanza, Mara, Dar es Salaam, Pwani,
Rukwa, Katavi, Manyara, Arusha, Songwe na Mbeya.
Awamu ya kwanza ilifanyika
tarehe 15 hadi 17 na ilihusisha watendaji kutoka mikoa ya Morogoro, Singida,
Dodoma, Kaskazini Unguja, Kusini Unguja, Mjini Magharibi, Geita, Kagera,
Mtwara, Lindi, Tabora, Kigoma, Tanga, Kilimanjaro, Ruvuma, Iringa na Njombe.
Mwisho.