
Jeshi la Polisi mkoa wa Rukwa limewakamata wanachama 11 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kwa tuhuma za kufanya mkusanyiko usio halali. Kati ya waliokamatwa, wanaume ni saba (7) na wanawake wanne (4), wakiwemo viongozi wanne wa chama hicho.
Viongozi waliokamatwa ni pamoja na:
Winfrida Joseph Khenani, Katibu Mwenezi wa Baraza la Vijana CHADEMA, Jimbo la Nkasi Kaskazini, Godfrid Bendera, Katibu wa CHADEMA, Jimbo la Nkasi Kaskazini, Evarist Mwanisawa, Katibu wa Baraza la Wazee CHADEMA, Wilaya ya Nkasi, Scolastica Mwalonde, Mwenyekiti wa CHADEMA, Kata ya Majengo
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi, viongozi hao walihusika katika kupanga na kushiriki mkusanyiko huo bila kibali.
Aidha, Jeshi la Polisi mkoa wa Rukwa linawataka Aida Khenani, Mbunge wa Jimbo la Nkasi Kaskazini, na Albeto John Kaliko, aliyekuwa Diwani wa Kata ya Itete, kujisalimisha katika Kituo cha Polisi wilaya ya Nkasi au Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai mkoani humo, kwa kuhusishwa na upangaji wa mkusanyiko huo.
Tufuatilie kupitia YouTube ya Global TV — usisahau ku-like, ku-comment na ku-subscribe ili uendelee kuhabarika kila siku kwa habari mbalimbali zenye ukweli na uhakika.