Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imetangaza RASMI majina ya wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi ikiwemo ubunge na uwakilishi, kwa ajili ya hatua za awali za kupigiwa kura za maoni. Kura hizo zitapigwa na wajumbe ili kumpata mgombea mmoja atakayebeba bendera ya chama hicho kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025.
CPA Amos MAKALLA Akizungumza na wanahabari Leo Julai 29 jijini Dodoma , ameeleza kuwa kwa upande wa Jimbo la Kigamboni, Dar es Salaam, majina sita yamepitishwa katika hatua ya awali ya uteuzi. Hata hivyo, jina la Mhandisi Hersi Said, ambaye pia ni Rais wa Klabu ya Yanga, halijarudi.