
“Ujumbe wa walinda amani wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo- DRC (MONUSCO) Umelaani vikali shambulio lililotokea usiku wa Julai 26 hadi 27, 2025, huko Komanda, kilomita 60 kusini magharibi mwa Bunia, mji mkuu wa Ituri”, taarifa ya MONUSCO kwa vyombo vya habari imesema.
Taarifa hiyo ya MONUSCO iliongeza kusema:” Kulingana na ripoti rasmi, shambulio la wanajeshi wa ADF lilisababisha vifo vya raia wasiopungua 43 wakiwemo wanawake 19, wanaume 15, na watoto tisa, huku watu kadhaa wakitekwa nyara.
Wizi ulifanyika na nyumba na maduka pia walichomwa moto waasi hao, na kuzidisha hali mbaya ya kibinadamu ambayo tayari inaripotiwa katika jimbo hilo.
Umoja wa Mataifa na Jeshi la Congo walisema kwamba raia waliokuwa wanahudhuria ibada ya mkesha katika kanisa la eneo hilo walikatwkatwa kwa mapanga, na kusababisha vifo vya watu hao na wengine kadhaa walijeruhiwa vibaya.
Luteni Jules Ngongo, Msemaji wa Jeshi la Congo katika jimbo la Ituri, ambako shambulio hilo lilitoke alisema jana Jumapili kupitia taarifa kwa vyombo vya habari iliyochapishwa kwenye mtandao wa X kwamba jeshi la Congo linasema mauaji haya yalitekelezwa na Allied Democratic Forces (ADF), kundi lenye silaha la kigeni linalotoka Uganda linaloendesha harakati zake katika jimbo wa Ituri.
Luteni Ngongo alisisitiza kuwa shambulio la mauaji hayo lilikuwa kitendo cha kulipiza kisasi kinacholenga kugeuza operesheni ya pamoja ya kijeshi inayoendelea inayowalenga ADF na Vikosi vya DRC na Vikosi vya Ulinzi vya Wananchi wa Uganda (UPDF).
Julai 23, 2025, MONUSCO iliwatuhumu ADF kufanya shambulio lingine lililowauwa raia 47 huko Eringeti, pia katika jimbo la Ituri, kati ya Julai 8 na 9, mwaka huu.
STORI NA ELVAN SITAMBULI