
Licha ya kushuka kwa viwango vya njaa duniani, ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa imeonyesha ongezeko la njaa barani Afrika. Takriban watu milioni 512 duniani wanatarajiwa kubaki bila chakula cha kutosha ifikapo mwisho wa muongo huu—asilimia 60 kati yao wakiwa Afrika.
Katika Mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Duniani uliofanyika Ethiopia chini ya Umoja wa Afrika, Katibu Mkuu wa UN António Guterres alionya kuwa chakula kamwe kisitumike kama “silaha ya vita.” Alisisitiza hitaji la hatua za haraka kukabiliana na mgogoro huo wa chakula.
Zaidi ya watu milioni 280 barani Afrika kwa sasa wanakabiliwa na utapiamlo, huku milioni 52 wakikabiliwa na ukosefu mkubwa wa chakula, na wengine milioni 3.4 wakiwa hatarini kuingia katika njaa kali. Viongozi walisisitiza umuhimu wa uwekezaji katika kilimo, ustahimilivu wa hali ya hewa, na mifumo ya ulinzi wa kijamii ili kunusuru bara dhidi ya janga hilo.
Tufuatilie kupitia YouTube ya Global TV — usisahau ku-like, ku-comment na ku-subscribe ili uendelee kuhabarika kila siku kwa habari mbalimbali zenye ukweli na uhakika.