
Meneja Mkuu Shirika la Masoko ya Kariakoo CPA Ashraph Abdulkarim (kushoto) akiwa na Mkurugenzi Mtendaji Shirika la Bima la Taifa Bw. Kaimu Mkenyenge (kulia) wakati wakisaini mkataba wa makubalinano ya utoaji huduma za bima kwa Soko jipya la Kariakoo litakalofunguliwa hivi karibuni hafla iliyofanyika Dar es Salaam leo 30 Julai 2025.

Meneja Mkuu Shirika la Masoko ya Kariakoo CPA Ashraph Abdulkarim (kushoto) akiwa na Mkurugenzi Mtendaji Shirika la Bima la Taifa Bw. Kaimu Mkenyenge (kulia) wakiwa wameshika hati za mkataba wa makubalinano ya utoaji huduma za bima kwa Soko jipya la Kariakoo leo 30 Julai 2025 Dar es Salaam mara baada ya kusaini.

Wajumbe wa timu ya Menejimenti ya Shirika la Bima la Taifa wakiwa kwenye hafla ya kusainiwa mkataba wa utoaji huduma za bima kwa Soko jipya la Kariakoo kati ya Shirika hilo na Shirika la Masoko ya Kariakoo leo 30 Julai 2025 Dar es Salaam.

Meneja Mkuu Shirika la Masoko ya Kariakoo CPA Ashraph Abdulkarim amesema lengo la kuingia makubaliano na Shirika la Bima la Taifa (NIC) ni kuwezesha Soko jipya la Kariakoo kuwa na huduma za bima ya majanga na kwamba wafanyabiashara wote watakaoingia watapaswa kukata bima.Hafla hiyo imefanyika leo 30 Julai 2025 Dar es Salaam. (Habari na Picha na Shirika la Masoko ya Kariakoo)