
Malkia wa mitindo na malkia wa vichwa vya habari, Zaiylisa, amhadhimisha siku yake ya kuzaliwa kwa kishindo hivi karibuni kwa staili ya kipekee na ya kuvutia. Katika kile kilichoonekana kama birthday hive ya karne, Zaiylisa hakusubiri zawadi—aliamua kujizawadia mwenyewe gari jipya aina ya Toyota Harrier, linalong’aa mithili ya almasi barabarani!
Lakini mambo hayakuishia hapo. Mrembo huyo alifanya photo shoot kali kandokando ya Harrier hiyo mpya. Kilichovutia zaidi? Alisimama pembeni ya gari hilo jipya likiwa karibu kabisa na gari alilowahi kununuliwa na ex wake maarufu, Haji Manara.
Katika picha hizo alizozipakia kwenye Instagram yake yenye mamilioni ya wafuasi, Zaiylisa aliandika: “Si kila unachopoteza ni laana, Wakati mwengine ni baraka ya kukufundisha mipaka…”
Hafla hiyo ya kuzaliwa pia ilihudhuriwa na rafiki yake wa karibu, Chris Outfit, ambaye naye hakuwa nyuma. Chris, ambaye ni mbunifu wa mavazi na mjasiriamali anayeinukia kwa kasi, alifika akiwa amependeza na kutinga kwa Mazda CX-5 mpya, aliyoipata kama zawadi yake binafsi kwa mafanikio ya mwaka huu. Wawili hao walionekana wakicheka, kupiga picha, na kusherehekea kwa moyo mmoja.