NA DENIS MLOWE, MAFINGA
MBUNGE aliyemaliza muda wake kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi katika jimbo la Mafinga Mjini, Cosato Chumi wa ubunge wa Jimbo la Iringa Mjini kupitia amewaongoza watia nia katika jimbo hilo kujinadi kwa wajumbe katika kata mbalimbali mjini hapa.
Chumi akiomba kura ya ndiyo ili kupata nafasi ya kuwania ubunge kupitia CCM katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025 kwa kipindi cha tatu ametaja mafanikio ambayo ameyafanya kwa kipindi alichokuwa mbunge na kuomba wajumbe wampe kura za ndio kuweza kumalizia miradi mbalimbali aliyoanzisha.
Alisema kuwa maendeleo ni hatua hayaji moja kwa moja hivyo kwa kipindi ambacho amekuwa Mbunge amefanikiwa katika sekta mbalimbali za afya kwa kutoa vifaa mbalimbali ikiwemo vitanda.
Alisisitiza kuwa ana dhamira ya kuwatumikia wananchi wa Mafinga mjini endapo atapata nafasi hiyo kutaja mafanikio katika kuboresha elimu, afya na miundombinu, akiahidi kushirikiana na wananchi kusukuma mbele gurudumu.
Akizungumzia wakazi wa kata ya Wambi waliomuuliza kuhusu maji alisema kuwa mradi wa maji wa bilioni 48 umeshaanza kujengwa hivyo wampe kura aendelee kusimamia katika kipindi cha miezi 12 mabomba yatakuwa yameshasambazwa hivyo kunufaisha wananchi wote wa mji wa Mafinga.
Chumi ambaye hadi anamaliza ubunge wake alikuwa naibu waziri wa Mambo ya Nje aliwashukuru wananchi kwa ushirikiano wao kipindi cha uongozi na kuwashukuru wajumbe kwa kumwamini na kuomba waendelee kumwamini.